Kurasa

Jumamosi, 19 Machi 2016

MITAJI KUTOKA TAASISI ZA FEDHA #CAPITAL FROM FINANCIAL INSTITUTIONS#

Hujambo mpenzi msomaji na  karibu tena katika mada zetu za ujasiriamali ambazo zimekuwa zikiletwa kwako kwa mfululizo maalum.

Leo tunaendelea na mada ambayo tayari tulishaianza ya Mitaji na vyanzovyake ambapo mala ya mwisho tuliishia kutoa mfano wa jamaa ambae alisafiri kutoka mkoani mpaka jijini Dar es salaam akiwa na nauli tu lakini bado alifanikiwa kuwa miongoni mwa watu wenye fedha mjini.

Katika muendelezo leo tutaangalia mitaji kutoka taasisi za fedha.


Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitegemea sana mitaji hii ambayo kama usipokuwa makini inaweza kukuletea matatizo makubwa.Mitaji hii ni ile ambayo mfanyabiashara huchukua kutoka taasisi za fedha kwa ahadi ya  kurudisha ikiwa na ongezeko maarufu kama riba.

Mala nyingi aina hii ya mtaji huambatana nadhamana ya mkopaji ambayo humlinda mkopeshaji endapo mkopaji anashindwa kurudisha fedha stahiki.Wafanyabiashara wengi wamejikuta nyumba pamoja na mashamba yao vinapigwa mnada kwasababu ya biashara zao ambazo zimetegemea aina hii ya mtaji kuanguka na hivyo kushindwa kulipia fedha iliyokopwa.

KUMBUKA;Umiliki wa biashara unategemea umiliki wa mtaji.Kama biashara yako asilimia kubwa mtaji wake unatokana na mikopo kutoka taasisi za fedha,wamiliki wa biashara yako wanakuwa ni taasisi hizo za fedha na sio wewe.Mala zote unapaswa kufikiria mtajhi wa aina hii wakati wewe ukiwa umeshajiimalisha kibiashara.Mtaji kutoka taasisi za fedha haupaswi kuzidi nusu ya mtaji wako binafsi ingawa unaweza kuzidi na bado ukafanikiwa kama utakuwa makini na biashara yako bila kuruhusu matumizi yasiyokuwa ya lazima.
Mala nyingi taasisi za fedha hutaka dhamana kama hati ya nyumba,Kiwanja,Leseni za biashra ama sleep za mshahara kwa wafanyakazi.

III.Mitaji kutoka ndugu jamaa na marafiki;

Mitaji hii hupatikana kwa kumuomba ndugu yako ambae ana akiba ya pesa za ziada.Katika aina hii ya mitaji unaweza kuambaiwa urudishe au la kulingana na mtu mwenyewe anaekupa mtaji huo.Pia aina hii huwa ni salama kutegemea na aina ya ndugu au jamaa anaekupa mtaji huo.

Mjasiriamali mzuri ni yule asieacha wazo lake la biashara kupotea bila kulifanyia kazi kama ni zuri na linaonekana lingeleta mafanikio.Hupambana kwa juhudi na maarifa kuhakikisha changamoto zinazomkwamisha kutimiza malengo yake zinapatiwa ufumbuzi na hatimae kuufikia mwisho unaokusudiwa.

Kumbuka kabla ya kuchukua mtaji sehemu fulani unapaswa kufanya utafiti kuona kama aina ya mtaji unaotaka kuuchukua ni sahihi au unaweza kukuletea matatizo.

PICHA;Mfanyabiashara akiwa kazini.

Mpendwa msomaji tumefika mwisho kwa leo.Kwa wale ambao ndio mala ya kwanza kusoma mfululizo wa machapisho haya mnapaswa kuanza kusoma post za mwanzo kuanzia Ujasiriamali ninini mpaka tulipoishia ili kupata muendelezo ulio makini.
Msisahau kuwa machapisho haya yanapatikana katika kitabu kinachouzwa kwa njia ya mtandao kwa shilingi 2500/= tu ambacho kipo kinaendelea kuuzwa.Kumbuka kitabu hicho kina mambo ambayo hayatachapishwa hapa kama jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama batiki na sabuni,jinsi ya kupata malighafi na bei za kila mali ghafi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni