Kurasa

Ijumaa, 25 Machi 2016

4.MAKAO YA BIASHARA.#BUSINESS CENTER#

Karibu tena mpendwa msomaji,ambae ni mfanyabiashara na wewe ambae unataka kuanza biashara au umeamua tu kujiongezea maarifa kuhusu biashara.Huu ni muendelezo wa mada zetu ambazo zinapatikana katika kitabu chetu kinachitwa MIMI NI TAJIRI kinachouzwa hapa kwa bei ya 2500/= tu.Kitabu hicho kina baadhi ya mambo muhimu ambayo hayachapishwi hapa kama vile jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama batiki,shampoo na nyingine zaidi ya nane,mahali ambapo unaweza kupata malighafi za kutengeneza bidhaa hizo na bei za malighafi husika.

Leo katika mada yetu tunaangalia makao ya biashara.



Makao ya biashara ni mahali au mazingira ambayo biashara ita au inafanyika.Inaweza kuwa jengo zima au chumba kimoja (flemu) kulingana na aina ya biashara.Wengine kukwepa ghalama biashara zao huzifanya bila kuwa na makazi maalum ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakitembea huku na kule kuudha bidhaa zao.Kuna aina mbalimbali za makao ya biashara;
1.Makazi ya mfanyabiashara.
2.Nyumba ya kukodi
3.Eneo maalum ya serikali

1.MAKAZI YA MFANYABIASHARA.
Hii ni nyumba au eneo la mfanyabiashara husika.Makao haya  huwa ni mazuri kwa biashara kwa kuwa hayana ghalama kulipia kila mwisho wa mwezi au mwaka.Hata hivyo makazi haya yanaweza kuwa na changamoto endapo eneo lilipo jengo la mfanyabiashara sio rafiki kwa biashara iliyokusudiwa.Inampasa mfanyabiashara kuanzisha biashara yake katika mazingira ambayo ni ya kibiashara bila kujali ni eneo la makazi yake au la.
2.NYUMBA YA KUKODI.
Huu ni utamaduni uliozoeleka na wafanyabiashara wengi.Baada ya mfanyabiashara kufanya utafiti na kuona mazingira yanayofaa kwa biashara yake hukodi nyumba au flemu kwaajili ya kuanzisha biashara katika eneo hilo.Njia hii huwa ni yi ya ghalama lakini humuwezesha mfanyabiasha kufikia malengo yake ya soko na hatimae kupata faida.
Maduka ya simu Kariakoo na mbwembwe za wauzaji
PICHA;Duka la simu Kariakoo.

3.ENEO MAALUM LASERIKALI.
Hili huweza kuwa jengo au eneo maalum ambalo serikali hulitenga kama soko.Ingawa njia hii huwa ina ghalama pia lakini ni ndogo ukilinganisha na eneo la kukodi la mtu binafsi.Pia huweza kumhakikishia mfanyabiashara soko kwani wateja wengi huwa wanatembelea maeneo haya kujipatia mahitaji yao binafsi na ya nyumbani.
PICHA;Soko kuu la Kariakoo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni