Kurasa

Alhamisi, 17 Machi 2016

MITAJI KATIKA UJASIRIAMALI

Hujambo mpenzi msomaji na karibu tena katika mfululizo wa mada zetu hizi za Ujasiriamali ambazo zinaletwa kwako na mimi mshauri wako wa mambo ya kibiashara MUKEBEZI DEONIDAS.Mada hizi zimechukuliwa kutoka katika kitabu ambacho kiko sokoni kwa sasa kinachoitwa MIMI NI TAJIRI ambacho huuzwa kwa shilingi elfu mbili na mia tano tu.Hata hivyo tunashukuru kwa muitikio wa watu wengi mnaoendelea kujinunulia kijitabu hiki chenye maarifa ya kutosha ikiwemo jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama batiki na nyingine nane za aina tofauti,Mahali yanakopatikana maduka ya malighafi pamoja na bei za malighafi hizo.Mada hizi tatu nilizozitaja hazitaweza kuchapishwa hapa na kwa hivyo wale watakaonunua kitabu hiki ndio pekee watakuta mada hizo au watakaonunua mada mojamoja ambazo huuzwa wa shilingi mia tano tu.Tumia mawasiliano yetu kama unataka kujipatia kitabu hiki au mada hizi zilizotajwa hapa.0654627227.

Leo tunakuletea mada inayohusu mtaji katika biashara au ujasiriamali

.
Mtaji ni kiasi cha pesa au kianzio katika biashara ambacho hutumiwa kuanzisha na kuendeleza biashara.Bahati mbaya n kuwa wajasiriamali wengi wamekuwa wakishindwa kufanya biashara kwasababu ya kukosa mitaji.

Mijadala mingi sana imefanyika na inaendelea kufanyika kwamba kati ya wazo la biashara na mttaji kipi ambacho huwa kinatangulia mwanzo.

Mjasiriamali mzuri ni yule ambae analitafakari vizuri wazo lake la biashara akilenga kuanzisha biashara inayotumia mtaji mdogo lakini ambayo itamletea faida kubwa.Mala nyingi biashara zenye mtaji mdogo lakini zenye malenngo ya kuleta faida kubwa inahitaji mtu mvumilivu sana hususani kwenye swala la muda.Kwa mfano jamaaa mmoja alikuwa na mtaji wa shilingi 20000/= mwaka 1999,alipofikiria wazo la biashara kwa mtaji wake akaona ni bora anunue eneo la ardhi halafu asubiri itakapopanda bei au thamani.Baada ya miiaka kumi aliweza kuuza eneo lile kwa shilingi milioni ishirini.

Najua hapo ulipo umeguna na kushusha pumzi.Umekuwa sio utamadunikwa sisi waafrika kuweka mipango ya muda mrufu kwasababu sio wavumilivu kusubiri matokeo mazuri na hiyo inasababisha watu wengi kuamini utajiri kupatikana kwa njia za panya.

AINA ZA MITAJI NA VYANZO VYAKE.
Kuna vyanzo mbalimbali vya mitaji lakini hivi vitatu vimekuwa vikitumika sana;
1.Rasirimali binafsi
2.Kutoka taasisi za fedha
3.Kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki

1. Rasilimali binafsi;
Huu ni mtaji unaotokana ni kile unachokimiliki.Mtaji huu huwa ni bora sana kuliko mingine.Wazungu wana msemo usemao 'tumia ulichonacho ili upate unachokihitaji' (Use what you have to get what you need) Jipe muda mzuri wa kuwaza na kutafakari una nini na unaweza kutumiaje ulichonacho ili kufikia malengo yako.Hakuna binadamu asie na kitu cha kuanzia.Bhati mbaya ni pale unapokuta msomi wa chuo kikuu anakuambia hana mtaji wakati huo akiwa na elimu ya degree au diploma pamoja na komputer mpakato yake ambayo huitumia kuangalia movie wakati akisubiri ajira ya laki nne.

Kila binadamu anetafuta maendeleo anapaswa kukitumia kichwa chake kama ilivyokusudiwa.Hakuna tofauti kati ya kufanya kazi za kuajiliwa na kazi binafsi.Kumbuka anaekuajilia anakuweka ili atumie ujuzi wako katika biashara yake na kujipatia faida.Sio lazima uwe na kitu kikubwa kwa mtaji binafsi.Jamaa mmoja ambae hutoa shuhuda sehemu mbalimbali alisafiri kutoka mbeya mpaka Dar es salaam akiwa na nauli pamoja na fedha kidogo za kujikimu.Alipofika ubungo hakujua aanzie wapi na akajikuta amekaa tu kituoni mpaka giza lilipoingia saa mbili usiku.Alienda kula kwa mama ntilie akarudi palepale alipokuwa amekaa na kupitiwa na usingizi.Alipoamka asubuhi alijikuta hata zile pesa ambazo alikuwa nazo zimeibiwa.Alipiga mahesabu akaona hana jinsi zaidi ya kuuza viatu vyake ambavyo bahati nzuri hakuibiwa.Kutokana na mauzo ya viatu hivyo alifanikiwa kupata elfu kumi.Jamaa yule aliulizia mahali ambapo angepata bidhaa za bei rahisi na akaelekezwa magari yaliyokuwa yanaelekea kariakoo.

Alipofika kariakoo jamaa yule alifanikiwa kununua mifuko kadhaa ya pipi na big jii ambazo aliamua kuziuza kwa wateja ambao walikuwa ni abiria wa mikoani pale ubungo mpaka mtaji wake ukakua maradufu.Pamoja na kwamba imepita miaka mingi sasa hivi jamaa yule yuko kariakoo anamiliki duka kubwa la pipi na biscuits akiziuza jumla kwa wafanyabiashara wa rejareja,akimiliki jumba kubwa la kuishi mbezi na mgari kadhaa.Maana ya mfano huu ni kuwa haijalishi una kidogo kiasi gani akili yako ndio maisha yako.

Mpenzi msomaji kwa leo tumefika mwisho wa sehemu ya kwanza ya mada yetu inayohusu mitaji.Wakati mwingine tutakuja kuendelea na mada hii ya mitaji katika sehemu ya pili na ya tatu.Usisahau kusoma mfululizo wa mada hizi kutoka mwanzo ili uweze kwenda na muendelezo sahihi na hatimae kuelewa nini kinachokusudiwa hapa.Hadi wakati mwingine

ASANTENI SANA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni