Kurasa

Alhamisi, 28 Mei 2015

JINSI YA KUTAMBUA KIPAJI CHA MTOTO WAKO NA KUKIENDELEZA.

 
 
Hujambo mpenzi msomaji na karibu sana katika mfululizo wa mafunzo kwa njia ya mtandao yanayoletwa na mimi muandishi wako Deonidas Mukebezi.Mafunzo haya pia yanapatikana kwa njia ya sauti kwenye mtandao wa watsapp ambapo yanatumika kufanya utafiti kuona kama ujumbe mmoja unaweza kuwafikia karibia watanzania wote na wasio waTanzania wanaotumia mtandao wa watsapp ili kuanzaisha kitu ambacho kitakuwa ni faida kubwa sana kwa watumiaji wa mtandao.Unachotakiwa kufanya ndugu msomaji unapopata ujumbe wa aina hii kwa njia ya sauti,ni kushare na wengine ili nao waweze kushare hatimae uwafikie waTanzania wote.
 
Tukirudi kwenye mada yetu kwanza tutaanza kuangalia maana ya neon kipaji;Huu ni uwezo anaokuwa nao mtu wa kufanya jambo Fulani bila hata kwenda kujifunza shuleni.Mala nyingi mtu huzaliwa na uwezo huo na anapokwenda shule kuuendeleza zaidi basi hulifanya jambo hilo kwa ufanisi sana.Sasa wewe kama mzazi unawezaje kutambua kipaji cha mwanao na kukiendeleza,fuatilia yafuatayo;
 
Kama motto wako anaongea kupita kiasi;Kuna watoto ambao huongea kwa spidi sana na huwa hawachoki kuongea.Watoto hawa huongea mpaka anapokwenda kulala na wengine huwa wanaongea mpaka usingizini.Huwa na tabia ya kusimulia visa mbalimbali au kukueleza mzazi yote yaliyotokea mchana pengine wakati wewe umeenda kazini au kwenye shughuli zako.Mpangilio wa maneno yao na sentensi huwa ni mzuri sana.Hii ni dalili nzuri sana kwa watoto hawa kama kipaji chao kitaendelezwa kwasababu fani zao mala nyingi huwa ni sharia,uandishi wa habari,uanasiasa pamoja na Mc wa majukwaani.
 
Jinsi ya kuwasaidia watoto wa aina hii;
1.Epuka kuwakatisha tama kwa yale wanayoongea na kama yanakera mfundishe kuongea yanayofurahisha.
 
2.Unaweza kumwambia akusimulie visa mbalimbali wakati wewe ukimrekodi na baada usikilize pamoja nae.Hii humjengea kujiamini na kuona kuwa anachofanya kinadhaminiwa.
 
3.Msaidie pia aweze kuwa msikilizaji mzuri kwa wewe kumsimulia wakati yeye akikusikiliza ana kumwambia arudie ulichosema.
 
4.Mtengenezee tabia ya kujiamini kwa kuepuka kumfokea au kumpiga mala kwa mala hususani kutokana na kosa la yeye kuongea sana.
 
Asante sana mpenzi msomaji wakati mwingine tutaangalia kipaji cha motto ambae kila jambo antaka kulifanya yeye tunawaita ''vimbelembele''.
Unaweza kuwasiliana na mimi kwenye namba yangu ya watsapp 0654627227 na tafadhali tuma ujumbe,hii ni kwa watsapp tu.

KANISA KATOLIKI LAJITOA KWENYE UCHAGUZI BURUNDI.

Kanisa Katoliki nchini Burundi limejiondoa katika mchakato mzima wa uchunguzi na uongozi wa aina yoyote katika uchaguzi huo.
Uamuzi huo umekuja wakati ikisalia wiki moja tu uchaguzi wa wabunge na madiwani ufanyike nchini humo
Kanisa katoliki ni kiungo muhimu katika suala la amani na demokrasia nchini Burundi tokea kuanzishwa mazungumzo ya amani ya Arusha mnamo miaka ya tisini.
EU inasema kuwa uamuzi wao umeafikiwa kwa sababu ya sheria kali dhidi ya vyombo vya habari na waandamanaji
Haya yamearifiwa wakati maandamano dhidi muhula wa tatu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza yanaendelea kufanyika katika mitaa kadhaa ya mji mkuu Bujumbura kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Wakati huohuo, Jumuia ya bara ulaya imesimamisha ujumbe wake uliokuwa usimamie uchaguzi mkuu nchini Burundi.
EU inasema kuwa uamuzi huo umeafikiwa kwa sababu ya sheria kali dhidi ya vyombo vya habari, matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji, na mazingara mabaya ya vitisho kwa vyama vya upinzani.
Rais Nkurunziza anapania kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu
Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki wakati wa ghasia za maandamano,
tangu rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mwezi uliopita kuwa anapania kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu, kinyume na katiba ya Burundi.
Uchaguzi wa urais umepangiwa kufanyika Juni tarehe tano, huku ule wa urais ukiwa mwishoni mwa mwezi huo wa Juni.
SHARED DIRECT FROM BBC SWAHILI

MWANAFUNZI ALAZIMISHWA KULA MATAPISHI YAKE .


Walimu wawili wamefukuzwa kazi baada ya kumlazimisha mwanafunzi kula matapishi yake baada ya kutapika wakati akipokea kipigo kutoka kwa walimu hao.

Walimu hao ambao walikuwa wanafundisha katika shule moja ya watoto wenye matatiza ya kihisia walitenda kosa hilo lililosababisha vibarua vyao kuota nyasi katika huko Suffolk county council.

Shule hiyo ambayo jina lake halikutajwa kwa sababu maalum imekuwa ikikumbwa na kashfa mbalimbali za kunyanyasa wanafunzi wake ambapo sasa matukio hayo yanafikia 100.

Kaisome The trent.

VIRUSI VYA KIMETA VYATUMWA KWENYE KAMBI ZA KIJESHI MAREKANI


Maafisa wakuu katika idara ya ulinzi ya Marekani wamekiri kuwa chembechembehai za ugonjwa hatari wa Kimeta zilitumwa kimakosa kwa kambi 9 za kijeshi nchini Marekani na moja nchini Korea Kusini.
Kulingana na makao makuu ya ulinzi nchini Marekani sampuli za chembechembehai za Kimeta zilidhaniwa kuwa zimekufa na hivyo zikatumwa kutumia njia ya usafirishaji mizigo ya umma kimakosa.
Chembechembe hizo za kimeta zilikuwa zimenuiwa kutumika katika mazoezi ya shambulizi la zana za kibaiolojia zakijeshi katika kambi za mazoezi.
Wandani wa maswala ya zana za kibayolojia wanasema kuwa kungetokea maafa makubwa iwapo chembechembe hizo za kimeta zingeachiliwa nje ya maabara maalum ya kibayolojia.
Maafisa wa serikali ya Marekani walioko Korea Kusini wameripoti kuwa takriban watu 22 waliogusana na zana hiyo katika kambi ya kijeshi ya Osnan wanachunguzwa.
Hadi sasa hakuna kati yao aliyeonesha dalili za maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
Wakati ukweli ulipobainika mahabara na vituo vya kijeshi vilifungwa.
Kimeta ni hatari ikinuswa au ikiliwa.
Ni silaha inayoweza kutumiwa wakati wa vita vya kemikali.
Makao makuu ya kijeshi ya Pentagon yanasema kuwa haijulikani ni watu wangapi wanaokabiliwa na hatari hiyo nchini Marekani.
Hadi uchunguzi ukamilike, hakuna bacteria zozote za kimeta zinaweza kusafirishwa kutoka Marekani.
Kambi za kijeshi zilizoathirika ni Texas, Maryland, Wisconsin, Delaware, New Jersey, Tennessee, New York, California na Virginia.
Kufikia sasa watu wanne pekee wanachunguzwa nchini Marekan
Shared directly from BBC SWAHILI.

JINSI YA KUTENGENEZA AIR FRESH


Tumekuwa mala nyingi na utaratibu wa kununua Air fresh na bidhaa nyingine kutoka nchi za nje kwa vigezo kuwa hatuwezi kutengeneza wenyewe au bidhaa zetu sio bora.Hapa nakuletea jinsi ambavyo unaweza kujitengenezea Air fresh yako mwenyewe na kuifanya nyumba yako kuwa na harufu nzuri tu.

Ili bidhaa yako ikamilike unahitaji baadhi ya vitu kama mvuke ambao umepoa.Hapa nina maanisha kuwa mvuke unapopoa untengeneza maji kwahiyo tunatakiwa kuwa na maji lakini lazima maji hayo yatokane na mvuke.

Unaweza kutengeneza maji hayo kwa kuchemsha maji kutunia pipa moja lililofungwa pande zote na kuwa na mrija au mpira unaotoka katika pipa hilo kuelekea kwenye pipa lingine ambalo liko pembeni.

Kwa mfumo huo maana yake ni kuwa mvuke kutoka pipa A unaotokana na kuchemka kwa maji utaelekea pipa B.Hakikisha unapata maji ya kutosha.

Uache mvuke katika pipa B upoe halafu anza kutengeneza kwa kuchukua maji lita ishirini uchanganye na harufu vijiko vinne vya chakula na ukoroge kwa dakika zisizopungua ishirini na tano.Ongeza tena maji lita kumi na ukoroge kwa dakika tano.Hapo Airfresh yako itakuwa tayari na weka kwenye containers kwaajili ya matumizi.

JINSI YA KUTENGENEZA DAWA YA KUSAFISHA VIOO


Dawa hii hutengenezwa kwa kutumia malighafi tatu ikiwemo sabuni ya maji, maji yenyewe pamoja na vinegar.

Alhamisi, 21 Mei 2015

WAWILI WAJITOA UCHAGUZI WA FIFA

Wagombea wawili kati ya wanne waliojitokeza kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la vyama vya soka Duniani FIFA wamejitoka katika kinyang'ang'anyiro hicho.
Nyota wa zamani wa soka huko Ureno , Luis Figo ambaye ni mmoja wa waliojitoa kuwania nafasi hiyo,amelalamikia mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi huo na kuiita kuwa ni wakinafiki.
Amesisitiza kuwa kwa mtazamo wake anaona kuwa taratibu zilizowekwa zililenga kumnufaisha mgombea mmoja tu na si kuelta usawa wa wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo,ambapo inaonekana kuwa ni mpango uliowekwa kumpatia nafasi ya ushindi Rais wa sasa Sepp Blatter ambaye anawania nafasi hiyo kwa kipindi cha tano.
Hata hivyo Rais wa chama cha soka huko Uholanzi , Michael van Praag , akijitoa. Huku wapinzani waliosalia ni Bw Blatter ambaye ni Jordan Prince Ali Al Hussein ambaye ni mwanachama wa kamati ya utendaji ya FIFA.
Mgombea mwingine aliyejitoa pia ni Rais wa chama cha soka cha Uholanzi Michael van Praag na hivyo kuwaacha Blatter na mtu anayedaiwa kuwa mpinzani wake wa karibu Prince Ali Al Hussein ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA

BBC SWAHILI.