Kurasa

Alhamisi, 28 Mei 2015

JINSI YA KUTENGENEZA AIR FRESH


Tumekuwa mala nyingi na utaratibu wa kununua Air fresh na bidhaa nyingine kutoka nchi za nje kwa vigezo kuwa hatuwezi kutengeneza wenyewe au bidhaa zetu sio bora.Hapa nakuletea jinsi ambavyo unaweza kujitengenezea Air fresh yako mwenyewe na kuifanya nyumba yako kuwa na harufu nzuri tu.

Ili bidhaa yako ikamilike unahitaji baadhi ya vitu kama mvuke ambao umepoa.Hapa nina maanisha kuwa mvuke unapopoa untengeneza maji kwahiyo tunatakiwa kuwa na maji lakini lazima maji hayo yatokane na mvuke.

Unaweza kutengeneza maji hayo kwa kuchemsha maji kutunia pipa moja lililofungwa pande zote na kuwa na mrija au mpira unaotoka katika pipa hilo kuelekea kwenye pipa lingine ambalo liko pembeni.

Kwa mfumo huo maana yake ni kuwa mvuke kutoka pipa A unaotokana na kuchemka kwa maji utaelekea pipa B.Hakikisha unapata maji ya kutosha.

Uache mvuke katika pipa B upoe halafu anza kutengeneza kwa kuchukua maji lita ishirini uchanganye na harufu vijiko vinne vya chakula na ukoroge kwa dakika zisizopungua ishirini na tano.Ongeza tena maji lita kumi na ukoroge kwa dakika tano.Hapo Airfresh yako itakuwa tayari na weka kwenye containers kwaajili ya matumizi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni