Kurasa

Alhamisi, 28 Mei 2015

JINSI YA KUTAMBUA KIPAJI CHA MTOTO WAKO NA KUKIENDELEZA.

 
 
Hujambo mpenzi msomaji na karibu sana katika mfululizo wa mafunzo kwa njia ya mtandao yanayoletwa na mimi muandishi wako Deonidas Mukebezi.Mafunzo haya pia yanapatikana kwa njia ya sauti kwenye mtandao wa watsapp ambapo yanatumika kufanya utafiti kuona kama ujumbe mmoja unaweza kuwafikia karibia watanzania wote na wasio waTanzania wanaotumia mtandao wa watsapp ili kuanzaisha kitu ambacho kitakuwa ni faida kubwa sana kwa watumiaji wa mtandao.Unachotakiwa kufanya ndugu msomaji unapopata ujumbe wa aina hii kwa njia ya sauti,ni kushare na wengine ili nao waweze kushare hatimae uwafikie waTanzania wote.
 
Tukirudi kwenye mada yetu kwanza tutaanza kuangalia maana ya neon kipaji;Huu ni uwezo anaokuwa nao mtu wa kufanya jambo Fulani bila hata kwenda kujifunza shuleni.Mala nyingi mtu huzaliwa na uwezo huo na anapokwenda shule kuuendeleza zaidi basi hulifanya jambo hilo kwa ufanisi sana.Sasa wewe kama mzazi unawezaje kutambua kipaji cha mwanao na kukiendeleza,fuatilia yafuatayo;
 
Kama motto wako anaongea kupita kiasi;Kuna watoto ambao huongea kwa spidi sana na huwa hawachoki kuongea.Watoto hawa huongea mpaka anapokwenda kulala na wengine huwa wanaongea mpaka usingizini.Huwa na tabia ya kusimulia visa mbalimbali au kukueleza mzazi yote yaliyotokea mchana pengine wakati wewe umeenda kazini au kwenye shughuli zako.Mpangilio wa maneno yao na sentensi huwa ni mzuri sana.Hii ni dalili nzuri sana kwa watoto hawa kama kipaji chao kitaendelezwa kwasababu fani zao mala nyingi huwa ni sharia,uandishi wa habari,uanasiasa pamoja na Mc wa majukwaani.
 
Jinsi ya kuwasaidia watoto wa aina hii;
1.Epuka kuwakatisha tama kwa yale wanayoongea na kama yanakera mfundishe kuongea yanayofurahisha.
 
2.Unaweza kumwambia akusimulie visa mbalimbali wakati wewe ukimrekodi na baada usikilize pamoja nae.Hii humjengea kujiamini na kuona kuwa anachofanya kinadhaminiwa.
 
3.Msaidie pia aweze kuwa msikilizaji mzuri kwa wewe kumsimulia wakati yeye akikusikiliza ana kumwambia arudie ulichosema.
 
4.Mtengenezee tabia ya kujiamini kwa kuepuka kumfokea au kumpiga mala kwa mala hususani kutokana na kosa la yeye kuongea sana.
 
Asante sana mpenzi msomaji wakati mwingine tutaangalia kipaji cha motto ambae kila jambo antaka kulifanya yeye tunawaita ''vimbelembele''.
Unaweza kuwasiliana na mimi kwenye namba yangu ya watsapp 0654627227 na tafadhali tuma ujumbe,hii ni kwa watsapp tu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni