Kurasa

Jumatano, 22 Oktoba 2014

MWANAFALSAFA ASEMA MUZIKI ANAOFANYA DIAMOND NI WA KIKI KWAHIYO NI KAWAIDA KUZOMEWA

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya maarufu kama Mwana Falsafa amesema kuwa Muziki aliozoea kuufanya Diamond ni muziki wa kiki kwahiyo ajue kuwa kuna kiki nzuri na kiki mbaya na kumtaka kuwa tayari kwa pande zote mbili kwakuwa ndio aina ya muziki aliouchagua.

Mwanafalsafa aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha xxl cha clouds fm na kutakiwa kuliongelea tukio lililompata msanii mwenzake wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul au Diamond plantinumz kama anavyofahamika na wengi.

Akiongea kwa mifano Mwanafalsafa alisema,tukio kama hilo liliwahi kuwakuta kipindi kile kukiwa na ushindani kati ya kundi lao la EAST COAST na lile la TMK WANAUME FAMILY ambapo alisema kuwa waliwahi kuzomewa na mashabiki wa kundi hilo na yeye binafsi ilimtetemesha sana na ilimjengea woga katika kazi hiyo ya muziki.

FA aliongeza kuwa inawezekana kabisa kukawa na mipango kutoka upande wa pili wa upinzani kukodisha watu ili wamzomee au kumbooo mpinzani na hivyo kumkatisha tamaa lakini katika hali ya kawaida msanii hatakiwi kukata tamaa kutokana na matukio hayo kwasababu hutokea kama ajari tu!.

Akizungumzia swala la wasanii kuwa na bifu Mwanafalsafa alisema kuwa kama wasanii husika wanajielewa basi bifu kati yao wanaweza kuitumia kutengeneza pesa na mambo mengine ya kibiashara lakini kwa msanii asiekomaa huichukulia kama personal na kuishia kutengeneza chuki ambazo hazina tija.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni