Kurasa

Jumatano, 22 Oktoba 2014

MENEJA WA DIAMOND AKAMATWA SAKATA LA KUVAA SARE ZA JWTZ,NEY NAE MATATANI

Diamond Platnumz, Nay wa Mitego na wasanii wengine waliovaa sare za jeshi kwenye show ya Fiesta Jumamosi iliyopita wapo matatani. Wasanii hao wamepewa amri na jeshi la polisi kuzirudisha wao wenyewe sare hizo kwenye kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kuna taarifa kuwa meneja wa Diamond, Babutale alikuwa akishikiliwa na polisi kuanzia jana japo tayari ameshatoka.
Nay wa Mitego amesema kuwa hata yeye anashangaa kuona jinsi mambo yalivyobadilika.
“Limekuwa tatizo kubwa sana,”amesema Nay.
“Kuna watu tu wajinga wanachochea hivi vitu ilimradi tu wote wawili mimi na Diamond tumeshapewa warning, tunatakiwa polisi kurudisha zile nguo na kupeleka tu vitu vya watu, tutazipeleka.”
“Babu Tale alikamatwa tangu jana, yupo polisi, tutajua nini cha kufanya kwa sababu nimeona Diamond naye alikuwa ananipigia kwahiyo sijajua watu wamempa ushauri gani, lakini hili suala linaisha tu. Unajua hatujafanyia uhalifu, tulikuwa kazini sawa maybe inawezekana tuna makosa lakisi sio zile nguo zote zilikuwa ni za jeshi, kwahiyo tutajua tu chakufanya tutapata tu jawabu,”amesisitiza Nay.
Pia Nay alizungumzia taarifa iliyotolewa ikidai kuwa walipata kibali cha kutumia nguo za JWTZ kwenye shughuli ile.“Ndiyo maana nakwambia kuna vitu vipo katikati hapa sisi wenyewe hatuelewi ni nini kinaendelea,”amesema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni