Kurasa

Alhamisi, 18 Septemba 2014

JINSI YA KUJENGA UHUSIANO NA WATU

Unaweza kuwa hujui kwamba kujenga uhusiano mzuri na wenzako au wafanyakazi wenzako kunaweza kukusaidia kufanikiwa kitaaluma na maisha yako kwa ujulma. Kwa makala hii utagundua kuwa muda mwingi unoutumia kwenye maisha yako ni kuwa pamoja na wafanyakazi wenzako hata kuliko na familia yako au kwingineko. Kuboresha mahusiano yako na watu ni vizuri kibiashara kwani inaongeza ufanisi katika eneo lako la kazi.
Kwa nyongeza ni makampuni machache ambayo watu wake wanafanya kazi bila kutegemea wengine ila makampuni mengi yanategemea watu kufanya kazi pamoja na watu hao hawawezi kufanya kazi pamoja kama hawana mahusiano mazuri.
Hivyo kuna njia tano za kuboresha mahusiano ninazozijua ingawa unaweza kuongeza za kwako kulingana na mazingira na uzoefu ulionao;
1. Unatakiwa kuwa muwazi, mkweli na mwenye kuwasiliana
“Linapokuja suala la mahusiano kazini au nyumbani na watu wanaokuzunguka unahitaji kuwa muwazi na mkweli kwa gharama yoyote hapo ndipo utakapofanikiwa, ” Nukuu kutoka kwa mwandishi mmoja aitwaye Harry.
Harry anasema hupenda kuwashauri watu kuwa wawazi na wakweli ili waweze kufanya kazi pamoja na kuwa ufanisi mkubwa. Ingawa wengine wanachukulia mazingira ya kazi ni sehemu ya kujionyesha, kufanya wanachotakiwa kufanya na kwenda nyumbani na wengine wanachukulia ni sehemu ambayo wanatumia nusu ya maisha yao na kujenga fulsa na kuboresha mahusiano kwa kiasi kikubwa.
2. Uwe ni mtu unayependeka
Wakati mwingine kuwa muwazi na mkweli peke yake hakutakupa mahusiano unayohitaji hivyo usikate tamaa. Unahitaji kuwa rafiki wa watu na mtu ambaye unajihusihsa kwenye matukio ya pamoja ya kijamii kazini. Kwa ufupi usiwe mtu wa kujitenga na watu wengine hata kama si watu wa rika yao au imani yako uwe na hekima ya kutosha kuweza kujihusisha nao kwa umakini na uelewa mkubwa bila kuathiri msimamo wako.
3. Unatakiwa kuwa mchunguzi au mwangalifu katika kujenga mahusiano
Kuna wengine wanajua jinsi ya kujenga mahusiano mazuri au bora kazini, kitu ambacho ninakushauri jaribu kuangalia na kuchunguza utamaduni wa hapo ofisini kabla ya kuchuakua hatua ya kwanza. Kama unaona italeta shida au huna uhakika wa kuwakaribisha wafanyakazi wenzako kwaajili ya chakula cha jioni unaweza kuanza na kuwakaribisha chakula cha mchana. Hautakuwa na mambo la kupoteza kwani inaanza kidogo kidogo halafu kitakuwa kitu cha kawaida.
4. Tafuta watu wenye mwelekEo sawa na wa kwako
Kwa watu wengine ni shida kuwa marafiki na wageni kabisa lakini kitu ambacho unatakiwa kujua marafiki ulionao sasa walikuwa wageni kwako kipindi fulani cha maisha yako. Ila kitu cha msingi kama kuna mambo ambayo mnafanana au mna mweleko mmoja ni rahisi kuanza mahusiano hapo kazini. Mfano watu ambao wanakunywa pombe hukutana bar au maeneo ya starehe, watu wa kanisani hukutana kanisani na wa msikitini hukutana huko na wenye kupenda michezo hukutana kwenye michezo. Hivyo unatakiwa kujua nanai anaendana na mfumo wa maisha yako.
5. Usiogope kufikiri makubwa au madogo
Siku zote ni rahisi kuanzisha mahusiano na watu ambao uko kwenye mazingira sawa kiuchumi au cheo. Haimaanishi kwamba huwezi kujenga mahusiano na watu walio chini yako au juu yako. Kinachobakia ni wewe mwenyewe kuchukua maamuzi binafsi katika kujenga mahusiano yako na watu wengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni