Kurasa

Ijumaa, 19 Septemba 2014

POLISI KWA HILI LA KUWAPIGA WAANDISHI MMEBORONGA

HILI LA POLISI KUWANYANYASA WAANDISHI HATUWEZI KUNYAMAZA HATA KIDOGO

Alhamisi ya tarehe 18 palitokea kutokuelewana kati ya polisi na wananchi wachache waliokuwa wamefika makao makuu ya polisi kwa lengo la kumsindikiza mwenyekiti wa chama cha Demoklasia na Maendeleo(CHADEMA),mheshimiwa Freeman Mbowe ambae aliitwa na polisi kwaajili ya mahojiano kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuchochea vurugu kwa kuitisha maandamano.

Sina haja ya kuzungumzia mgogoro huo kati ya polisi na Mwenyekiti wa CHADEMA na wafuasi wake kwa kuwa mambo hayo ni ya kisheria na sijui ni nani yuko sahihi na nani hayuko sahihi.

Kilichonisikitisha katika tukio lile ni kitendo cha Askali wa Jeshi la polisi kuamua kuwashambulia waandishi wa habari kana kwamba hawakuwa na haki ya kufanya kazi yao!

Ni juzi tu serikali kupitia makamo wake wa Rais imetoka kuongea na wahariri na kusisitiza uhusiano mzuri kati ya taasisi za serikali likiwemo jeshi la polisi na vyombo vya habari.

Nina imani kubwa kuwa serikali ilifanya hivyo ikijua kuwa waandishi ni kundi kubwa sana katika nchi ambalo linaweza kuiamulia nchi kwenda kushoto au kulia.

Ni wazi wanajua kuwa waandishi ni kundi ambalo likiamua nchi isitawalike haitawaliki na wakiamua nchi itawalike inatawalika.

Waandishi wanaweza kuligeuza jambo dogo kabisa kwenye utawala likawa kubwa na kubadilisha kabisa hali ya hewa..

Hii ina maana kuwa kundi hili la waandishi lina nguvu kuliko pengine hata hao polisi lakini wanajua taaluma yao na kuheshimu taaluma nyingine na ndio mana nchi inaendelea kuwa na amani mpaka leo.

Tuna mifano ya waandishi ambao wametumia taaluma yao kuzibadilisha nchi na kuleta maafa makubwa kama KENYA na RWANDA,kwahiyo kama vile ambavyo waandishi wanaheshimu taaluma nyingine nao pia wanapaswa kupewa heshima stahiki na kulindwa ipasavyo kama taaluma ambayo ni hatari sana umakini usipokuwepo na taaluma ambayo ikitumiwa vizuri inaweza kusukuma maendeleo haraka sana nchini na kudumisha amani.

Nimeamua kuandika haya yote nikiwa na fikra kuwa pengine taasisi hii ya jeshi la polisi imesahau wajibu na haki ya muandishi!,au pengine wanaidharau taaluma ya uandishi kutokana na kutokuwa na ufahamu juu ya kile ambacho waandishi wanaweza kukifanya, au pengine wameigeuza heshima ya waandishi kwao kuwa utumwa.

Naomba niwakumbushe polisi kurudi kwenye mstari na kujua wajibu na haki za makundi mbalimbali katika jamii.Waandishi wanalindwa mpaka vitani vipi kuwanyanyasa kwenye vimatukio vya kawaida ka hiki cha Mbowe!!!Acheni bana hilo jipu mnalililemba siku moja litatumbuka!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni