Kurasa

Jumanne, 5 Agosti 2014

RASIMU YA KATIBA INAPOKA MADARAKA YA WATAWALA WASEMA MTANDAO WA WANAFUNZI

Mtandao wa wanafunzi Tanzania umesema kuwa chanzo cha mgogoro unaoendelea kati ya wajumbe wa bunge maalum la katiba ni kutokana na ukweli kwamba rasimu ya sasa ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ina muelekeo wa kuwapokonya madaraka watawala ambayo walipewa katika katiba ya zamani na kuyarudisha kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,Katibu wa mtandao huo wa wanafunzi bwana ALPHONCE LUSAYO alisema kuwa katiba ya zamani ilikuwa ni zao la watawala ambapo tar 16 march 1977 chini ya Rais Julius Kambarage Nyerere katiba hiyo ilitungwa na watu ishirini tu ndani ya masaa manne chini ya uenyekiti wa aliekuwa katibu wa ASP Shekh Thabit Kombo.

Alisema Tofauti kubwa imeonekana katika rasimu ya katiba ya sasa ambayo ni zao la watawaliwa inayoshirikisha mawazo ya wananchi wengi na kuleta msuguano ndani ya Bunge maalum la katiba.

Hata hivyo Mtandao huo umesema kuwa kuna dhambi ambayo ni ya kihistoria na haitaweza kufutika katika mioyo ya watanzania na haitaweza kusuluhishwa kwa maridhiano endapo mchakato wa kupata katiba mpya uliogharimu mabilioni ya Watanzania utakwama.

Aidha mtandao uliwataka wajumbe kuachana na maslahi ya makundi yao na kuwaka malengo ya pamoja ya kupata katiba mpya ambayo itakuwa ni katiba ya wananchi na sio katiba ya kikundi flani cha siasa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni