Kurasa

Jumatano, 6 Agosti 2014

MAHAKAMANI KWA UBAKAJI


Turn off for: Swahili
Na Deonidas Mukebezi, Dar es Salaam
MKAZI wa Mbezi Luis Omary Kupaza (32), amefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni akikabilikwa na kosa la kumbaka mtoto
(jinalimehifadhiwa) mwenye umri wa miaka (14),
Akisomewa kosa lake jana mbele ya Hakimu Izhaq Kuppa, wakili wa
Serikali Masin Mussa, alidai kuwa tukio hilo lilitokea Disemba 2013
huko eneo la Mbezi Msigwa.
Musa alidai kuwa Mshtakiwa alimbaka mtoto huyo kisha kumsababishia
maumivu makali sehemu za siri.
Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo bado
haujakamilika ambapo Hakimu Kuppa alidai kuwa kwa mujibu wa shtaka
hilo linadhaminika kisheria hivyo alimtaka mshtakiwa awe na wadhamini
wawili wenye barua ya utambulisho pamoja na nakala ya vitambulisho
vyao pia watakao saini ya maandishi ya Sh laki tano kila mmoja.
Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa katika Mahakama hiyo mara baada ya
mshtakiwa kushindwa kutimiza vigezo vilivyoainisha na Hakimu. Kesi
hiyo imeahirishwa hadi Agosti 19 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika hatua nyingine,Meneja wa kituo cha mafuta cha Gudal kilichopo
Ubungo Kibangu pamoja na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UCC-UDSM), wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kinondoni wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuiba fedha
taslimu Sh. Milioni 51.6 mali ya Kituo hicho.
Washitakiwa hao ni Meneja Saadi Mohamed (21)na Edwin Mbuya (21) ambao
ni wakazi wa Ubungo Kibangu Jijini Dar es Salaam.
Wakisomewa mashtaka yao jana mbele ya Hakimu Kwey Rusema, Wakili wa
Serikali Credo Rugaju, alidai kuwa katika shtaka la kwanza,
linalowakabili washtakiwa hao ni kula njama ya kutenda kosa ambapo
tukio hilo lilitokea kati ya tarehe na muda usiyojulikana maeneo ya
Kinondoni Wilayani hapo.
Katika shtaka la pili Wakili Rugaju alidai kuwa Julai 28 mwaka huu
washtakiwa waliiba fedha taslimu Sh 51,689,500 mali ya kituo cha
mafuta cha Gudal kilichopo Ubungo Kibangu.
Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na upelelezi tayari umekamilika
hivyo upande wa Jamhuri uliomba Mahakama hiyo iwape washtakiwa dhamana
kwa kuwa ni haki yao kisheria.
Hata hivyo Hakimu Rusema alidai kuwa kila mshtakiwa anatakiwa awe na
wadhamini wawili kwa kila mmoja na kati yao awe na hati ya mali
isiyohamishika au kuweka saini ya maandishi ya Sh Milioni 15.
Washtakiwa walirudishwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya
dhamana na kesi hiyo itakuja tena Agosti 19 mwaka huu kwa ajili ya
kusikilizwa maelezo ya awali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni