Kurasa

Jumatatu, 4 Agosti 2014

MANSOOR AKAMATWA NA SIRAHA NA RISASI ZAIDI YA 500

Zanzibar.-Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mansour Yusuph Himid amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume na sheria imefahamika visiwani humo jana.
Mansour ambaye alivuliwa uanachama wa CCM na kupoteza nafasi ya mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Kiembesamaki, alikamatwa nyumbani kwake huko Chukwani na kufanyiwa upekuzi mkali na askari wa kikosi cha upelelezi wakiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Jeshi hilo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar Salum Msangi alisema Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za kiintelejensia kuwa waziri huyo wa zamani anamiliki silaha kinyume na sheria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni