Kurasa

Jumamosi, 17 Mei 2014

RATIBA YA MAZISHI NA WASIFU WA MTOTO WA MKURUGENZI OFISI YA RAIS.

Saturday, May 17, 2014
RATIBA YA MAZISHI YA PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU, NA WASIFU WAKE
MAZISHI LEO JUMAMOSI TAREHE 17.05.2014
SHUGHULI ZOTE ZITAFANYIKA NYUMBANI KWA BW. SALVA RWEYEMAMU KINONDONI, MKABALA NA VIJANA HOSTEL NA MANGO GARDEN, JIJINI DAR ES SALAAM
SAA 1.00: ASUBUHI KIFUNGUA KINYWA - NYUMBANI
SAA 4.00-5.00: CHAKULA CHA MCHANA - NYUMBANI
SAA 5.00-6.00: KUAGA MWILI - NYUMBANI
SAA 6.00-7.00: MISA KATIKA KANISA KATOLIKI MWANANYAMALA
SAA 8.00 Mchana: SHUGHULI ZA MAZISHI MAKABURI YA KINONDONI
---------------------------------------------------------------
WASIFU WA PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU
[image]Rwechungura Brian Salvatory Rweyemamu, aliyefariki dunia alfajiri ya juzi, Alhamisi, Mei 15, 2014 ni mtoto wa kwanza wa Salva Rweyemamu na Isabella Kafumba Rweyemamu. Alizaliwa Desemba 27, mwaka 1987, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar Es Salaam.
Alipata elimu ya awali katika Shule ya Awali ya Mama wa Kiganda, Kinondoni na Kwa Mama Kate eneo la Chang’ombe, Dar es Salaam kabla ya kuhamia Kenya ambako alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Top Hill na Lukenya. Hatimaye alihamia kwenye mji Mkuu wa Ubelgiji wa Brussels ambako aliendelea na elimu ya msingi mwaka 1996.
Brian alijiunga na shule ya Bweni ya Trinity Exeter nchini Uingereza ambako aliendelea na kumalizia elimu ya msingi. Ili kumrudisha katika mazingira ya Kitanzania, Bwana Brian alirudia tena darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Julius Nyerere iliyoko Mbezi Beach, Kinondoni, Dar Es Salaam, mwaka 1998.
Alijiunga na Shule ya Sekondari ya St. Albans ya mjini Pretoria, Afrika Kusini, mwaka 1999, ambako alikaa miaka minne kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kaboja nje kidogo ya mji mkuu wa Uganda wa Kampala ambako alimaliza kidato cha sita mwaka 2005.
Alijiunga na Chuo Kikuu nchini Malaysia ambako alichukua masomo ya International Trade, masomo ambayo yalikuwa bado yanamdai credits za semester ya mwisho kabla ya kuaga dunia.
Alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Mlale, Songea, 2010 na kumaliza kumaliza mafunzo yake mwaka 2011 na hatimaye alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) ambako alifanya na kumaliza mafunzo katika Kambi ya Mafinga mjini Iringa mwaka 06/12/2013 kabla ya kuajiriwa na JWTZ mwishoni mwa mwaka jana.
Aliomba na kupewa likizo yake ya kwanza ndani ya JWTZ wiki mbili zilizopita ambako alikaa nyumbani kwa siku chache kabla ya kushambuliwa na malaria kali wiki iliyopita. Alilazwa Jumamosi iliyopita tarehe 10/05/14 katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo akiwa na malaria na kupoteza fahamu.
Alianza kupata fahamu kwa mbali siku ya Jumanne usiku na kujaribu kuongea siku ya Jumatano.
Via:Michuzi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni