Kurasa

Alhamisi, 3 Aprili 2014

MBINU SITA ZA KUISHI NA KUMHANDLE BOSS MKOROFI


Bila shaka ni ukweli usiopingika kuwa ili kazi iweze kufanywa vizuri,ni lazima anaefanya kazi hiyo aipende na aifanye kwa moyo wake wote.Pia ni kweli kuwa ofisi yako ndio mahali ambapo unakaa muda mrefu zaidi kuliko mahali pengine ukiondoa kitandani.Kwa bahati mbaya wafanyakazi wengi wamejikuta wakizichukia sehemu zao za kazi kutokana na aina ya mabosli walionao.Badala ya kufanya kazi kwa moyo,mtu anajikuta anafanya kazi kuepuka purukushani za bosi na kimsingi kazi hiyo haiwezi kufanywa kiufanisi ukilinganisha na kama mtu huyo anaeifanya angeifanya kwa moyo.Kuna mabosi wengi ambao hawajawahi kuwaamini wafanyakazi wao na mala nyingi maamuzi yao wanayafanya kwa hisia badala ya kufikilia.Mabosi hawa ni hataru sana kwani wanaweza kukufanya ukaharibu kazi yako na huwa ndio namba moja kukufukuza kazi.

Pamoja na ukweli wote huo bado unatakiwa kufanya kazi yako kiufanisi ili kuijenga profession yako.Kwahiyo ili kumuepuka bosi mkoarofi,anaefoka ovyo,na ambae anaendeshwa na hisia,hizi ni hatua sita unazoweza kuzitumia kuishi na mabosi wa aina hiyo.

1.ANDIKA KILA KITU AMBACHO KINAHUSIANA NA BOSI WAKO.
Hakikisha kila mnachojadiri au kufanya na bosi wako unakiweka kwenye maandishi ili kiwe kumbukumbu nzuri atakapokuwa anakushutumu vitu ambavyo utakuwa na uhakika kuwa ni maagizo yake.Mala nyingi mabosi wa aina hii huwa ni wasahaulifu kwa kuwa hawatumii sana akili zao bali hutumia hisia kufanya maamuzi.Kutokana na hilo hawakubali kirahisi utetezi wa mtu isipokuwa kama kuna ushahidi ambao unaonekana.Hakikisha wakati unaandika kumbukumbu zako hizo anakuwa hayupo ili kuepusha matatizo zaidi.

2.EPUKA KUKASIRIKA AU KUONESHA SURA YOYOTE YA KUKASIRIKA WAKATI BOSI WAKO AKIWA AMEPANIC.
Unapoona bosi wako amekasirika au anabwabwaja ovyo kuwa mtulivu na uoneshe tabia zako za kitaaluma(professional manner)ulizofundishwa shule.Tatizo ni kuwa watu wengi huwa wanasahau mambo ya taaluma na kufanya mambo kwa mazoea.Utakapokuwa mtulivu bosi wako atagundua kuwa anachokifanya ni utoto na anaweza kutulia.Pia epuka kujadiliana nae ishu ya kazi akiwa amekasirika kwa kuwa mnaweza kuharibi kazi.Mwambia hatuwezi kujadili ishu hii ukiwa katika hali hiyo.

3KUBALIANA NA SHUTUMA ZAKE KUMRIDHISHA.
Bado naongelea kuhusiana na kuwa professional.Ukitaka kumuweza bosi wa aina hii usipambane kwa kubishana nae,yaani usilipe neno kwa neno.Hii inamaana kuwa usikatae kile anachokiongea bali msikilize halafu umwambie kuwa unakubaliana na shutuma zake na utazifanyia kazi,lakini na wewe pia una matatizo ambayo anapaswa kuyasikiliza.Hii inaweza kumpunguza jazba kuliko ukikataa kila anachosema jambo ambalo linaweza kuleta matatizo zaidi,kumbuka yeye ndio bosi.

4.TAMBUA KUWA HUWEZI KUMBADILISHA BOSI WAKO KAMA NDIO TABIA YAKE KIBIOLOGIA ISIPOKUWA MPE TAARIFA.
Ukigundua kuwa ukorofi ndio tabia ya bosi wako na wala sio ya kuiga kiasi kwamba inaweza kubadilika,unapaswa kuishi kulingana na hali hiyo na mbinu mojawapo ni kuhakikisha kuwa unampa taarifa za matatizo yako at least awe anayafahamu ili asisingizie kuwa hayajui.

5.BAKI KUWA PROFESSIONAL NA USIBADILIKE KWA SABABU YA UKOROFI WWA BOSI.
Kuwa mtulivu na fanya mambo yote kulingana na taaluma yako inavyotaka.Hii haijalishi kuwa anakasirika au la kwa kuwa ukifanya kulingana na taaluma ni dhahili kuwa kazi itakuwa nzuri na sio vinginevyo na hakuna bosi aliewahi kumfukuza kazi mtu aliefanya kazi nzuri.

6.USIMPANDE KICHWANI BOSI WAKO KWA KUWA HII ITAZAA UADUI KATI YAKO NA BOSI WAKO.
Epuka kung'ang'ania jambo hata kama ni haki yako kwani hii itamfanya bosi wako akukasirikie maradufu na kujenga uadui kitu ambacho kitakufanya uione kazi chungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni