Kurasa

Alhamisi, 3 Aprili 2014

MWANAJESHI AWAUA WENZAKE 3 MAREKANI.

Wanajeshi wanne wamepigwa risasi na kuuawa katika kambi ya jeshi huko Fort Hood jimboni Texas.

Jenerali Mark Milley, amesema mwanajeshi mmoja ndiye aliyewafyetulia wenzake risasi hizo karibu na zahanati ya afya ya kijeshi ya Carl R Darnall iliyoko katika kambi hiyo ya Jeshi.

Watu watatu walifariki kabla ya mwanajeshi huyo kujipiga risasi na kujiua.

Wanajeshi wapato wanne wanatibiwa majeraha mabaya ya risasi.

Daktari mkuu wa zahanati hiyo Dakta Glen Couchman anaelezea majeraha wanayotibu.

''Wote walikuwa na majereha mbalimbali ya risasi kwenye vifua shingo na tumbo''.

Waziri wa usalama Chuck Hagel amesema kuwa uchunguzi tayari umeshaanza kubaini chanzo cha kisa hicho cha pili kuikumba kambi hii.

''ninajua kuwa mtangulizi wangu Leon Pannetta aliwahi kusema kuwa tukio kama hili mwaka wa 2009 litachungzwa .

Ni wazi lazima kuna kitu kinachoendelea ambacho hakifai.

Lazima tutatue shida hii .''

Rais Obama amehuzunishwa sana na tukio hilo ambalo anasema limetokea katika kambi ambayo inapaswa kuwa salama .

Obama amesema ''amezungumza na maafisa wa FBI na idara ya mahakama kutafuta kwa kina kiini cha makabiliano haya ilikuhakikisha kambi zetu zimekuwa salama.

Hii siyo mara ya kwanza kwa kituo hicho kikubwa cha majeshi ya Marekani Fort Hood kushuhudia ufyetulianaji wa risasi .

Mwaka 2009 wakati dakatari wa magonjwa ya kiakili wa jeshi la Marekani meja Nidal Hasan alipowapiga risasi na kuwaua watu kumi na watatu.

Rais Obama amesema anafuatilia yanayotukia katika kambi hiyo kwa makini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni