Kurasa

Alhamisi, 3 Aprili 2014

MBINU ZA KUFANYA ONE ON ONE INTERVIEW

ONE ON ONE Interview ni moja kati ya mbinu zinazotumiwa kujua mambo ambayo yanawapa watu flan msukumo katika maisha.Hii inahusiana na mambo anayoyapenda mtu,maisha yao,passion na mahusiano yao.Aina hii ya majadiliano inahusiana na kuondoa ubaguzi kwa mtu pamoja na kutokumuhukumu mtu na badala yake kumsikiliza kwa makini na kwa lengo la kupata uhalisia

Ili kugundua vizuri self interest za watu unaowahoji unahitaji kuwasikiliza kwa makini kwa kuzingatia lugha za mwili,sauti za hisia pamoja na mabadiliko katika macho yao.Pia unapaswa kufahamu na kutambua kinachowapa watu unaowahojimsisimko na kuwatia nguvu.Lengo kuu la aina hii ya interview ni kutoa ujuzi kwa jamii.Maana yake ni kwamba unapata interest kwa mtu unaemhoji na kufanya taarifa hizo zitumiwe na watu katika jamii.

MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA WAKATI WA ONE ON ONE INTERVIEW.

1.JIANDAE.
Fikiria kuhusiana na kitu unachotaka kukifahamu na kifanye kiwe kifupi ili isiwe ya kukera.

2.IFANYE IWE INFORMAL.Aina hii ya interview ni tofauti na interview nyingine kama za kazi,au za ki academic au survey.Katika interview hii unakuwa huna maswali maalum ya kuuliza bali unakwenda na jinsi masimulizi yanavyokwenda hususani kwa kuangalialugha za mwili,historia na vyanzo vya taarifa.

3.ANGALIA MUUNGANIKO WA MATUKIO.
Wakati unafanya aina hii ya interview jaribu kutafuta mambo ambayo yanaunganisha matukio.Kwa mfano unaweza kuhusisha baadhi ya mambo na uzoefu wako katika eneo husika ingawa hupaswi kugeuka kuwa msimuliaji isipokuwa mlengwa ndio anatakiwa kuchukua nafasi kubwa.

4.ULIZA MASWALI YA MOJA KWA MOJA.
Epuka kuuliza maswali yenye mzunguuko na yasio eleweka.unaweza kuuliza maswali kwa mfano 'umejifunza nini kutokana na hilo?' au 'Kwanini umekuwa makini sana katika swala hilo?'

5EPUKA MASWALI YA NDIO AU HAPANA.
Maswali haya hayatoi maelezo ya kina,na kama ni muhimu kuyauliza basi ni vizuri swali linalofuata likawa kwanini?.

6.KUWA MSIKILIZAJI MZURI.
Jaribu kukipa uhai kile ambacho tayari kimesemwa na mtu unaemhoji.Mala nyingi watu wanapata moyo wa kuendelea kujieleza kwa undani wanapogundua kuwa wanasikilizwa kwa makini tafauti na wanapogundua kuwa wanachokiongea hakieleweki kwa wanaemsimulia.

7KUWA NA UHAKIKA KUWA UNAMUELEWA MUONGEAJI.
Kuhakiki kama unaelewa au la jaribu kurudia kile anachokisema muongeaji na kuuliza kama ni sawa au la.

8.MWISHO ANGALIA MATOKEO YA MAHOJIANO YAKO.
Hii inakusaidia kujua ulichokifanya sawa na unachotakiwa kuboresha wakati mwingine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni