Kurasa

Jumatano, 23 Aprili 2014

DAWA ZASITISHWA KUTENGEZWA KWA SABABU WASANII KUZITUMIA KAMA DAWA ZA KULEZWA

Wednesday, April 23, 2014
Matumizi mabaya ya dawa ya kifua kwa asanii yasababisha kutokutengenezwa tena kwa dawa hizo
Kampuni ya kutengeneza dawa za kikohozi"Actavis" yasitisha uzalishaji na mauzo ya dawa za"Promethazine Codeine"na kuziondoa katika sok, kutokana na matumizi mabaya ya dawa hizo kwa wasanii wengi wakubwa wa Marekani.
Msemaji wa kampuni hiyo amesema kutokana na attention kubwa iliyotolewa na vyombo vua habari Actavis imetoa uamuzi wa kusitisha uzalisha na mauzo ya dawa hizo.msemaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa attention hiyo imeipamba matumizi ya dawa hizo ambayo ni kinyume na sheria na hatari ambayo ni tofauti na matumzi halali ya dawa hizo.
Kabla Actavis haijaondoa dawa hizo, thamani ya dawa hizo mtaani kwa chupa yalifikia mpaka dola 800 lakini mtu wa karibu wa soko la dawa hizo ameiambia TMZ kuwa ma-Rapper kwa sasa wamefikia kutoa ofa kichaa ya kununua kila kilichobaki, na kuwa msanii maarufu tayari ameshatoa ofa kwa dealer ya kufikia dola laki moja kupata kile anachoweza.
cha kuchekesha na kuonyesha ubobeaji wa matumizi mabaya ya dawa hizo, Soulja Boy amepost picha ya chupa 6 za dawa hizo siku ya jumatatu kuonyesha kupungua kwa madawa hayo sokoni na kuandika
"Soulja got the juice. They say the streets dry. I say you gotta be kiddin me. I serve everybody."
Justine Bieber na Soulja Boy wameonekana kuwa ndio watumiaji wazuri wa dawa hizo, na kutokana na uamuzi wa kampuni hiyo sasa itakula kwao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni