Kurasa

Jumanne, 22 Aprili 2014

CHIDI BENZI UKIFULIA KIMZIKI NDIO UNAPIGA WATU.

Tuesday, April 22, 2014
Chidi Benz ashikiliwa na polisi baada ya kumjeruhi vibaya Ex girlfriend, afikishwa mahakamani
Msanii wa Hiphop anaeiwakilisha Ilala, Chidi Benz anadaiwa kushikiliwa na polisi mwishoni mwa wiki baada ya kumpiga na kumjeruhi vibaya mwanadada anaejulikana kama Mwanaisha ambae anadaiwa kuwa ni mpenzi wake wa zamani.
Kwa mujibu wa Chidi Benz amesema yeye alikuwa akipita nje ya bar iliyo karibu na kwake ilala Flat alipokuwa akirudi nyumbani kwake akiambatana na mpenzi wake wa sasa ndipo aliposkia sauti ikimuita na kumuuliza zaidi ya mara tatu
" chidi naona uko na mama watoto" kusogea karibu akakuta ni Mwanaisha na wenzake, ndio akamwambia mbona unanichora au kwasababu nipo na dem mkali kuliko wewe unaona wivu, kilichofata ni chupa ambayo Mwanaisha aliirusha ikampata kichwani na kumpasua damu zikatoka ndipo yeye alimshika nywele Mwanaisha na baada ya hapo kilichofata hakumbuki maana alikuwa amelewa.
Chidi Benz anashikiliwa na polisi na leo hii kesi imeenda mahakamani ambapo hakimu ameamuru kuendelea kushikiliwa kwa Chidi baada ya hali ya mwanaisha kuwa mbaya kiasi cha kushindwa kuongea.
Mwanaisha ameshonwa nyuzi 18 mdomoni, uso umeumuka na kichwa kimemvimba sana.
zaidi msikilize Gossip Cop hapo chini Mwanaisha Iddi mkazi wa Ilala Dar es salaam, dada aliyepigwa na Chidi Benzi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni