Kurasa

Jumanne, 22 Aprili 2014

KESI YA MRAMBA BADO..

KESI YA MRAMBA YAPIGWA KALENDA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imepiga kalenda kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7 kwa matumizimabaya ya madaraka leo aprili 22, hadi hapo itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia amri iliyotolewa Novemba 20, mwaka 2013 itakavyotekelezwa yakutoa misamaha ya kodi, inayowakabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na wenzake ya matumizi .
Mapema mwaka jana Jopo la mahakimu watatu linalosikiliza kesi hiyo, likiongozwa na Jaji John Utamwa, lizitaka pande zote mbili Jamhuri na utetezi katika kesi hiyo, kuwasilisha hoja za kisheria, baada ya kukataliwa kwa shahidi wa wa tatu wa utetezi, aliyekuwa Kamishna wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Felician Busigara.
Wengine katika jop hilo ni, Jaji Sam Rumanyika ambao walianza kusikiliza kesi hiyo kabla ya kupanda wadhifa na kuwa majaji na msajili Saul Kinemela. Busigara, alipokuwa akitoa ushahidi wa upande wa utetezi, alizua mvutano wa kisheria kuhusu ushahidi aliokuwa anatoa ulijikita kwenye utaalam badala ya kuhusika na kesi ya msingi na upande wa mashtaka uliwasilisha pingamizi la kumkataa shahidi huyo.
Kutokana na mvutano huo, jopo hilo liliamuru pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za kisheria kuhusu ushahidi wa shahidi huyo. Mbali na Mramba washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.
Akiahirisha kesi hiyo, Jaji Rumanyika alisema jopo halijakamilika na kwamba wajumbe wengine wana udhuru wa kikazi hadi leo itakapotajwa na kuangalia kuhusu amri iliyotolewa na mahakama hiyo itatekelezwa vipi.
Mramba na wenzake, wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni