KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Kurasa
▼
Jumanne, 11 Februari 2014
TUWAHESHIMU VIONGOZI WETU WA NCHI.
KUTOKA KWA MHARIRI.
Deonidas Mukebezi;Mhariri wa blog hii.
Katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 18 kifungu kidogo cha 1 kinampa kila mtu ambae ni raia wa Tanzania uhuru wa kutoa maoni bila kubughudhiwa na mtu.Ibara hiyo pia inampa mtu uhuru wa kusambaza,kupokea au kutoa taarifa zozote kupitia chombo chochote cha kusambaza na kupokea habari.Kama hiyo haitoshi ibara hiyo pia inampa mtu uhuru wa kutokuingiliwa katika taarifa zake binafsi.
Hata hivyo katika katiba hiyohiyo ya jamhuru ya muungano wa Tanzania ibara ya 30(1) inasema kuwa haki na uhuru hautatumiwa na mtu katika misingi kwamba zinaingilia haki na uhuru wa mtu mwingine.Pia kifungu cha pili cha ibara hiyo kinasema kuwa provission zinazotengeneza na kufanya hakina uhuru,havizuii utekelezwaji wa sheria za nchi au kuzuia sheria mpya zilizotungwa kufanya kazi.
Nimeanza na kidokezo hicho cha katiba kwasababu watu wengi wamekuwa wakijisahau na kutamka au kuposti mambo ambayo ni kinyume kabisa na malengo ya uhuru wa kujieleza.Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la picha nyingi za viongozi zikitumwa katika mitandao mbalimbali,facebook,instagram, na mingine ambazo zinawaonesha viongozi hao wakiwa katika hali ambazo hazikubaliki kimaadili.Baadhi ya picha zimekuwa na ujumbe unaomuonesha kiongozi husika akihamasisha watu kutokufanya kazi.Hii ni hatari sana.Tunapaswa kujua kuwa mtu anapoachwa kuwa huru kufanya chochote akitakacho maana yake anajitambua na pia anajua kujicontrol
Tuwaheshimu viongozi wa nchi kwa kuwa kuna watu wanaheshimu sana kile anachosema kiongozi,hii ina maana kuwa mambo mengine yanakuwa na adhari moja kwa moja kwa jamii.
HIZI HAPA NI BAADHI YA PICHA AMBAZO ZIIMETUMWA KATIKA MITANDAO MBALIMBALI.TUACHE TABIA HII.
Kweli hatari kaka
JibuFuta