KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Kurasa
▼
Jumamosi, 22 Februari 2014
SHULE 10 ZILIZOSHIKA MKIA KATIKA MATOKEA YA KIDATO CHA NNE
Siku zote katika maisha kuna wa kwanza na wa mwisho ,kauli hii inajidhirisha mara baada ya NECTA kutangaza matokeo ya kidato cha nne nchini huku kukiwa na shule zilizoshika nafasi za juu na zile za zilizoshika mkia.
Kwa upande wa shule 10 za mwisho kwenye kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 40, shule ya kwanza ni Kisima ya Pwani, Kitongoni ya Kigoma na Tongoni ya Tanga.
Nyingine ni Njechele ya Dar es Salaam, Lumemo ya Morogoro, Mvuti ya Dar es Salaam, Tambani ya Pwani, Nasibugani ya Pwani, Ungulu ya Morogoro na Kitonga ya Dar es Salaam.
Shule za mwisho kwenye kundi lenye watahiniwa chini ya 40 ni Singisa ya Morogoro, Hurui ya Dodoma, Barabarani ya Ruvuma, Nandanga ya Lindi na Vihokolo ya Mtwara.
Nyingine ni Chongoleani ya Tanga, Likawage ya Lindi, Ngwandi ya Dodoma, Rungwa ya Singida na Uchindile ya Morogoro
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni