KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Kurasa
▼
Jumanne, 4 Februari 2014
KUFUNGIWA VIDEO YA SNURA 'NIMEVURUGWA'KUMEONDOA TATIZO??
Hivi karibuni taarifa zilizagaa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kufungiwa kwa video ya wimbo wa msanii snura wa Nimevurugwa kwa kile kilichoonekana kuwa ni video ambayo haiendani na maadili ya kitanzania.
Inawezekana ikawa ni kweli haiendani na maadili ya kitanzania na hivyo jamii ya kitanzania itakapoangalia inaweza kupotoka hususani watoto wadogo na wanafunzi wa shule.
Lakini najaribu kujiuliza,na pengine hata msomaji wangu utakuwa unajiuliza maswali mengi,swali mojawapo likiwa,Hii BASATA inakuwaga wapi mpaka video inatoka na kusambaa mitaani na wao kukurupuka huko waliko na kusema video imefungiwa ikiwa tayari iko katika mitandao,ma CD pamoja na maeneo mbalimbali.
Kingine cha kujiuliza,ni kweli ni kwasababu ya maadili au kuna sababu nyingine,kwani nakumbuka kuna video nyingi tu ambazo wanacheza katika mitindo hiyo ya snura na hazifungiwi,mfano mzuri ni video ya IT bata,au hata Besta kuna wimbo alikuwa katika mazingira hayo hayo na hakufungiwa!
Au kwasababu ya kile kipande cha wimbo alichoponda nchi kuyumbayumba?mtazamo tu jamani,naruhusiwa na katiba kutoa maoni yangu katika ibara ya 18(1).
PICHA ZA SNURA AKIWA KATIKA POZI MBALIMBALI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni