Kurasa

Jumanne, 4 Februari 2014

ARSENAL YAPANDA KWA MGONGO WA CHELSEA


Timu ya soka ya ligi kuu ya uingereza Arsenal maarufu kama the gunners,jana ilijikuta ikibaki kileleni mwa ligi hiyo kwa tofauti ya point mbili mbele ya manchester city na chelsea baada ya hapo jana chelsea kuifunga manchester city kwa goli moja kwa sifuri katika uwanja wa Etihad.

Gori hilo pekee la chelsea lilifungwa na mshambuliaji wake Ivanovic katika dakika ya 32 na kudumu kwa kipindi chote cha mchezo huo ambao kila timu ilitaka kushinda ili kujiwekea mazingira mazuri katika ligi hiyo ambayo imeonekana kuwa ngumu kuliko ligi zote hasa msimu huu ambapo timu hizo zimepishana kwa pengo la poit chache sana na hivyo kila timu kujitahidi kuongeza mbinu za ushindi

Katika msimamo wa ligi hiyo kwa sasa Arsenal inaongoza ikiwa na point 55,ikifuatiwa na manchester city yenye point 53 na iliyoizidi chelsea kwa magori lakini timu hizo mbili zikiwa na point sawa.

Bahati mbaya ipo kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo ambao wako nyuma ya vinala kwa point 15 hasa mala baada ya kupoteza mechi mwishoni mwa wiki.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA YA MECHI YA MANCHESTER CITY VS CHELSEA

NAVAS AKIJITAHIDI KUMKIMBIA MCHEZAJI WA CHELSEA


JOE KATIKA HARAKATI


GAME NGUMU YAYA TOURE




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni