Kurasa

Jumatatu, 3 Februari 2014

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM KITENGO CHA HABARI WACHANGANYWA NA MITIHANI.

Wanafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam shule ya habari na mawasiliano(SJMC)wapo katika wakati mgumu kwa sasa hasa mala baada ya kuanza kwa mitihani ya semister ya kwanza katika chuo hicho.
.
Wakizungumza na muandishi wa habari hii kwa nyakati tofauti wanafunzi wa chuo hicho walisema kuwa kila mmoja kwa sasa yuko bisy na mitihani ili kuhakikisha kuwa anajiweka katika nafasi nzuri ya kutokurudia mitihani mwezi wa tisa na kutengeneza ufaulu mzuri utakaompa unafuu katika soko la ajira hapo baadae.

Mmoja kati ya wanafunzi chuoni hapo ambae anasoma kitengo cha habari(journalism) bwana YUSUF NURU alionekana kuhangaika huku na huko katika makundi mbalimbali yaliyokuwa yanahaha kujadili somo ambalo lilitarajiwa kufanyika leo saa tano asubuhi.

Moja kati ya vitu ambavyo wanafunzi huviogopa sana ni mitihani hiyo ikifuatiwa na matokeo ya majaribio mbalimbali darasani ambayo hujumlishwa na kupata matokeo ambyo mwisho wa semister huchanganywa na matokeo ya mtihani wa mwisho na mwanafunzi anakuwa amevuna alichopanda kwa semister nzima.

Blog hii inawatakia wanafunzi hao mtihani mwema na wenye mafanikio na mwisho wa siku chuo hicho kitengeneze waandishi wazuri watakaokuwa tegemeo kwa taifa hili changa.

PICHA;WANAFUNZI WAKIWA WAMEJUMUIKA KWA UPENDO.


PICHA HII NI MOJA KATI YA PICHA ZA WHATSAPP AMBAZO WANAFUNZI WAMETUMIANA KATIKA KUNDI LAO KAMA MOJA YA UTANI NA KUPEANA MOYO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni