Kurasa

Alhamisi, 16 Januari 2014

TUTUMIE RASILIMALI ZETU KUPAMBANA NA UMASIKINI

Mala kadhaa nimekuwa nikijiuliza kwanini nchi kama Tanzania inakuwa maskini kiasi cha wananchi wake kuishi chini ya dora moja kwa siku.Umaskini huo ambao kwa wale ambao wako kwenye nchi nyingine za magharibi kama nchi za bara la Ulaya na Amerika ya kusininchi wanashangaa kutokana na rasilimali nyingi tulizobalikiwa na mwenyezi Mungu.Tuna milima mikubwa kama mlima kilimanjaro ambao ni wa pili kwa urefu duniani,tuna mbuga mbalimbali za wanyama kama serengeti na nyingine ambazo zimekuwa zikivutia mamia ya watalii kila mwaka na kuingizia nchi yetu fedha za kigeni.

Swali la kujiuliza ni kwa nini tumeendelea kuwa maskini pamoja na yote hayo tuliyobalikiwa?Au pengine uongozi wetu hauna ubunifu wa kutosha katika kutumia rasilimali hizikuwa vyanzo vya mapato?Au pengine fedha zinapatikana lakini baadhi ya watu wachache wameamua kujilimbikizia wao wenyewe bila kuwakumbuka watanzania ambao ndio wanastahili maslahi hayo?

Napata shida sana kuona pamoja na kushindwa kuwa mikakati ya maana ya kuzibadilisha rasilimali zetu ili ziweze kuongeza pato la taifa na hatimae fedha kwenda kwa wananchi ili waweze kujikwamua na umaskini,baadhi ya watu wameamua kuwaua wanyama na kuuza viungo vyao zikiwemo pembe na ngozi.Matukio mbalimbali ya kuua ndovu na kusafirisha pembe zake yamekuwa yakiripotiwa na baada ya hatua kuchukuliwa watanzania wengine hawaonekani kushtuka na wamekuwa wakiendelea na matukio hayo.

Tunapaswa kujua kuwa wale ni viumbe hai na kama tutaendelea kuwaua ni wazi kuwa watakwisha na hivyo tutakuwa tumetupa zawadi nzuri kabisa aliyotupa Mungu.

Watanzania tunapaswa kuishi kwa kufikilia maisha ya watoto wetu na sio maisha yetu binafsi.Tukumbuke kuwa hata baada ya sisi kuondoka katika dunia hii tutaacha vizazi vyetu na watahitaji kuendelea kufaidi matunda ya rasilimali hizi alizotutunukia Mungu

Tazama baadhi ya picha zinazoonyesha mamba wanaopatikana wilaya ya Bagamoyo ambao wanawakilisha utajili tulionao Tanzania na ambao kama tutautumia nchi hii itakuwa na maendeleo ya hali ya juu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni