Kurasa

Alhamisi, 16 Januari 2014

TUJIHADHARI NA MATAPELI HAWA

siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi kubwa la matapeli wa mtandaoni ambao wanatumia mtandao kujipatia fedha za watanzania kwa njia zisizo halali na moja kati ya kundi hilo ni kundi linaloojiita JAKAYA FOUNDATION ambao hutumia jina la rais kuwarubuni watanzania kuwa wao ni taasisi ambayo hutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa watanzania.

Muandishi wa habari hii alipoangalia taasisi hiyo katika mtandao alikuta wameweka vigezo ambavyo vinaweza kumfanya mtu akakopeshwa ambavyo ni pamoja na kuwa na kitambulisho na kuwa ni mtanzania,pia walipotoa mawasiliano walisema kuwa wanapatikana katika majengo ya wizara ya utumishi wa umma,jengo namba tatu, ghorofa ya kwanza,chumba namba sita,idara ya mikopo.

Baada ya kupata taarifa hizo muandishi wa habari hii alifunga safari kuelekea posta katika ofisi za utumishi wa umma ambapo alikutana na wahusika walioonekana kushangazwa na habari hizo na kudai kuwa ofisi hizo hazina mikopo ya aina hiyo na hao ni matapeli wanaotumi aidara hiyo kujipatia fedha isivyo kihalali.

Nilijaribu kumuuliza mhusika ambae jina tunaliweka kapuni kwa sababu za kiusalama kwanini watu hao walichagua ofisi hizo na sio ofisi nyingine kufanyia utapeli,alisema kuwa yeye hajui kitu chochote kuhusiana na swala la watu hao.

Baada ya kufuatilia kwa undani zaidi muandishi wa habari hii aligundua kuwa taasisi hiyo ilikuwepo muda mrefu na baadhi ya watanzania tayari walishatuma ada pamoja na michango mbalimbali ambayo baada ya kujiunga ndio mtu anakuwa mwanachama kamili kiasi cha shilingi elfu arobaini na tano,fedha ambazo mtu anapaswa kuzituma kupitia namba ya tigo pesa.

Watu hao pia wamejaribu kuhusisha makampuni makubwa ya simu kama vodacom,airtel pamoja na tigo,pia wameihusisha benki kuu ya tanzania katika mladi huo.

Tulipojalibu kumpigia simu kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi ilala simu yake iliita tu bila kujibiwa.

Uongozi na waandishi wote wa DOUBLE LL KIDS wanapenda kuwatahadhalishs watanzania na kampuni hizi uchwara na kuwa wanapopata taarifa katika mitandao waende eneo husika wakaulize kwanza kabla ya kufanya jambo lolote ambalo litawasababishia hasara

Pia tunaiomba serikali kuwa makini na vikundi hivi kwa kujaribu kutafuta wataaramu wa IT wawe wanatoataarifa kama hizi ambazo husababisha watanzania wengi maskini kutapeliwa bila kujijua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni