Kurasa

Alhamisi, 16 Januari 2014

REMIX YA NO1 YA DIAMOND YAFIKISHA WATAZAMAJI 200000 NDANI YA WIKI MOJA.

Katika hali ya kushangaza na ya kutia matumaini kwa wasanii wa music wa kizazi kipya wa ndani ya nchi,wimbo wa namba1 remix wa msanii Nasib Abdul maarufu kwa jina la Diamond umeweza kufikisha watazamaji laki mbili katika mtandao wa youtube ndani ya wiki moja tangu wimbo huo ulipotoka.

Wimbo huo ambao ni remix ya wimbo wake wa kwanza alioimba peke yake wa namba 1 ambao wenyewe umefikisha watazamaji zaidi ya milioni moja katika mtandao wa youtube,amemshirikisha msanii nguli wa Nigeria Davido ambae anatamba na stail yake ya skelewi.

Katika wimbo huo wa namba1 remix wasanii hao wameamua kuchanganya stail mbili tofauti za kucheza za ngororo ya Diamond na Skelewi ya Davido.

Huu ni muendelezo mzuri wa msanii Diamond wa kuhakikisha kuwa anakuwa muimbaji wa kimataifa na hatimae kuongeza soko la muziki wa kizazi kipya ujulikanao kama "bongo flava"ulimwenguni.

Wingi wa watazamaji wa kazi ya msanii katika mtandao huo wa you tube ni kigezo kizuri sana cha kupima kama kazi ya msanii imekubalika au la na hili linadhihirishwa pale ambapo msanii mwingine wa Tanzania Baby Madaha alipoomba kumshirikisha msanii sean paul katika wimbo wake na msanii huyo akamjibu kuwa kama anataka kushirikiana na yeye basi wimbo wake uwe na angalau watazamaji elfu kumi youtube.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni