Kurasa

Alhamisi, 16 Januari 2014

MICHAEL SCHUMACHER KUBAKI KATIKA COMA MAISHA YOTE.

By mukebezi Deonidas

Mwanamichezo aliefanikiwa zaidi katika mbio za magari zaformula1(F1)Michael Schumacher 44 anahofiwa kubaki katika hali ya coma na madaktari ambao wanamsimamia katika matibabu yake.

Bingwa huyo ambae alipata ajali ya kuanguka wakati anafanya michezo ya kuteleza(skiing)huko ski resort katika French alps mwezi wa kumi na mbilitarehe 29 na kofia ngumu aliyokuwa amevaa kupasuka na kugawanyika vipande viwili,anahofiwa kubaki katika hali hiyo maisha yake yote baada ya madaktari kusema siku ya jumatano kuwa watu waliopata matatizo makubwa katika kichwa kama schumacher wamekuwa na matatizo ya kudumu ambayo hupelekea mgonjwa kuwa na matatizo ya kiakili.

"Wagonjwa ambao hupatwa na tatizo la coma huwa mala nyingi wanaamka baada ya wiki moja au mbili,hata hivyo tatizo la schumacher linaonekana kuwa kubwa kutokana na kuwa hajaamka kwa siku kadhaa sasa ambazo zinaweza kupelekea akapata matatizo ya kudumu ya ubongo"walisema wanasayansi siku ya jumatano.

Schumacheramekuwa katika coma kwa siku 18 sasa na madactari wamesema kuwa hajapata nafuu ya kutosha kuamshwa kwa sasa,baada ya kuwekwa katika hali hiyo ili kuruhusu aweze kupata nafuu kutokana na tatizo alilolipata.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni