Kurasa

Jumatano, 15 Januari 2014

DIVA,B 12 NA MCHOMVU WATIMULIWA CLOUDS

Watangazaji wa redio maarufu nchini Clouds FM,Adam Mchomvu,Loveness Malinzi(Diva)na Hamisi Mandi (B12)wamesimamishwa kazi kwa muda usiojulikanakutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kutokuhudhulia maadhimisho ya sherehe za miaka kumi na nne ya kituo hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi bwana Ruge Mutahaba alisema watangazaji hao wamekuwa wakifanya makosa mbalimbali yanayo pingana na sera na taratibu za kituo hicho na kwa kwamba uongozi umeshindwa kuvumilia tabia hizo na kuamua kuwasimamisha kazi.

"Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja,ila naomba nieleweke kuwa kila ofisi ina taratibu zake ambazo zinapaswa kufuatwa na hawa watangazaji wamevunja sera na taratibu zetu,hivyo hatukuwa budi kuchukua hatua"alisema Ruge.

Watangazaji hao waliofanikiwa kujikusanyia washabiki wengi nje na ndani ya nchi ya Tanzania wamesimamishwa kwa muda usiojulikana wakati uongozi unajaribu kufuata taratibu nyingine kabla ya kujua cha kufanya dhidi yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni