Kurasa

Jumatatu, 6 Januari 2014

ZITO AIGAWA CHADEMA






Na deonidas mukebezi

Katika hali ya kushangaza leo mahakama kuu ya Tanzania,badala ya wananchi kushuhudia upinzani uliozoeleka kati ya vyama viwili vya siasa,leo upinzani ulikuwa kati ya wafuasi wa chama kimoja cha CHADEMA wengine wakiwa upande wa mbunge wa kaskazini kwa tiketi ya chama hicho bwana Zito Zuberi Kabwe,na wengine wakiwa upande wa chama.

Wakiongea na blog hii baadhi ya wafuasi wa zito walisema kuwa hawaondoki pale mahakamani mpaka wafahamu hatima ya kiongozi wao huyo hata kama itabidi kutumia nguvu

Kwa upande wa wafuasi wa CHADEMA walisema kuwa wale wanaojifanya ni wafuasi wa Zito,hawakuwa wanachama wa kweli na hata kama utamwambia mmoja wao akupe kadi,hatakupa kwakuwa hawana kadi na ni wafuasi wa kununuliwa kwa pesa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni