Kurasa

Jumatatu, 27 Januari 2014

PICHA ZA WATU AMBAO NI MOST HANDSOME DUNIANI

HUYU NI MJUKUU WA MFALME FAISAL WA SAUDIA


WA PILI HAPA CHINI NI HRITHIK ROSHAN MCHEZA FILAMU WA INDIA

WA TATU NI IMRANI ABASS MUIGIZAJI WA PAKSTAN

WA NNE NI TARKAN,MUIMBAJI WA UTURUKI

WA TANO NA WA MWISHO NI FAZZA MUEMERITI

Labda unaweza kujiuliza kwanini nimeamua kukupa habari hii.Au mwingine anaweza kusema Mukebezi amefikiria nini;Nilichofikiria ni kutaka kukuonesha jinsi saikolojia ilivyo na nguvu na kuwa ukifanikiwa kuwashika watu saikolojia zao una kuwa na uwezo wa kuwafanya na kuwaambia chochote.Katika orodha ya watu mia moja wazuri kuliko wote duniani,hakuna hata muafrika mmoja!cha ajabu ni kuwa hata sisi waafrika wenyewe tunaamini hivyo!Haya ni matokeo ya kushikwa kisaikolojia na wazungu toka zamani kiasi kwamba sasahivi kila anachofanya mtu wa nchi za magharibi kinaonekana kuwa cha maana.

Wito wangu kwa WAAFRIKA wenzangu ni kuanza kujikubali wenyewe na kuvitangaza vya kwetu badala ya kuamini kila kinachosemwa na watu wa nchi za magharibi.Kutokana na wao kutushika sisi kisaikolojia wanatufanya soko la bidhaa zao na sisi tunaendelea kuwa wachuuzi na wapiga debe wa bidhaa za kigeni.TAFAKARI VIZURI!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni