Kurasa

Jumanne, 28 Januari 2014

MAFURIKO MOROGORO YAMEIKUMBUSHA SERIKALI JUKUMU LAO

Moja katika majukumu ya serikali yaliyoorodheshwa katika katiba ni kuwapatia wananchi huduma ya chakula,Hii ni moja kati ya huduma za jamii ambazo serikali inapaswa kulitekeleza siku zote ambazo inakuwa madarakani.Cha kushangaza ni kuwa serikali huwa inasubiri majanga makubwa kama hili lililotokea juzijuzi mkoani Morogoro la mafuriko.

Shukrani kwa Rais JK kuwaagiza watumishi kuhakikisha kuwa waathirika wanapata chakura kutoka kwenye maghara ya serikali.

Lengo la kipengere hiki ni kutaka kuwakumbusha kuwa matatizo ya njaa katika jamii yapo kila siku,na ni jukumu la serikali kutafuta nani ana njaa na kuhakikisha kuwa anapata chakula.

Niwape pole sana wale walioathiriwa na mafuriko pale Morogoro na kuwapa moyo kuwa Serikali yao haijawatupa na msaada wa kutosha unatarajiwa ili kuyapunguza maumivua ambayo yalitarajiwa

.

Baadhi ya picha zikionesha tukio la mafuriko Morogoro na madhara yaliyojitokeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni