Kurasa

Jumanne, 28 Januari 2014

ARSENAL WAVUTWA SHATI

Viongozi wa ligi ya uingereza timu ya soka Arsenal jana walijikuta wakipoteza point mbili baada ya kukubali kutoka sale na timu ya soka ya Southompton.

Timu hiyo ya southompton ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia mchezaji wake Jose Fonte,baada ya kuunganisha cross kali iliyotoka kwa mchezaji Luke Shaw.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika ubao ulikuwa unasomeka kuwa ni moja kwa sifuri.

Kipindi cha pilli kilianza kwa kasi,Arsenal wakishambulia kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa wanarudisha gori na pengine kupata lingine la ushindi,na juhudi zao zilionekana dakika ya 48 wakati Bakari Sagna alipochonnga cross kali iliyounganishwa moja kwa moja gorini na mchezaji Olivia Giriud.

Iliwachukua tena Arsenal dakika nne tu kufunga bao la pili kupitia mchezaji wake Saint Carzola baada ya kupiga shuti lililomzidi nguvu goal keeper wa Southampton na kufanya ubao usomeke 2-1 mpaka kufikia dakika ya 52.

Sherehe ya magori katika mechi hiyo ilifungwa dakika ya 52 wakati Adam Lallana alipofunga goli la kusawazisha baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa mchezaji mwenzake Jay Rodriges na kuuvurumisha langoni mwa Arsenal na kukamilisha kalamu hiyo.

Katika mechi hiyo Arsena walijikuta wakicheza pungufu kuanzia dakika ya 80 baada ya mchezaji wao Matheau Flamin kupewa kadi nyekundu iliyotokana na kumchezea rafu ya miguu miwili mchezaji wa timu pinzani Morgan Shneiderlin


Matokei ya mechi nyingine zilizochezwa jana ni;

MANCHESTER UNITED 2-0 CARDIFF


SWANSEA 2-0 FULHAM


CRISTAL PALACE 1-0 HULL CITY

NORWICH CITY 0-0 NEWCASTLE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni