KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Kurasa
▼
Jumatatu, 20 Januari 2014
KUMBE FROLA MVUNGI ALITAMANI DIAMOND NA WEMA WARUDIANE!!
Zikiwa zimepita wiki kadhaa tangu wasanii maarufu wa Tanzania Nasib Abdul maarufu kama Diamond na Wema Sepetu kurudiana,imebainika kuwa baadhi ya wasanii wa Tanzania walikuwa wakitamani uhusiano huo urudi na moja kati ya wasanii hao ni msanii Frola Mvungi.
Hilo lilibainika baada ya muandishi wa habari hii kuinyaka moja kati ya ujumbe wa maneno wa Frola Mvungi alioutuma katika mtandao wa instagram akiwaombea wasanii hao kwa Mungu waendeleze uhusiano huo.
"Mimi na mume wangu tunapendana sana,but still tunaipenda sana hii couple iendelee kuwepo Mungu awajalie mapenzi tele wafike malengo.All the best darling."ulisema ujumbe huo wa Frola.
Uhusiano wa wasanii hao wawili umeonekana kurudi kwa nguvu zaidi ya zamani na watu wengi ambao ni wapenzi wa wasanii hao wameonekana kufurahia uhusiano huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni