Kurasa

Jumatatu, 20 Januari 2014

UMEME WAPANDISHA BEI ZA BIDHAA BAGAMOYO

Katika hali ambayo iliwasikitisha wananchi wengi mjini Bagamoyo,wafanyabiashara wameamua kupandisha bei za bidhaa mbalimbali zikiwemo zile za huduma za saloni na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali.

Wakizungumza na muandishi wa habari hii,wafanyabiashara hao wamesema kuwa wao sio wanaosababisha ugumu wa maisha kwa wateja bali shirika la umeme na serikali kwa ujumla ndio wa kulaumiwa kwa kupandisha bei ya umeme bila kuzingatia hali za watanzania wengi

"Sisi bwana hatuwezi kulaumiwa kwa hili,unapopandisha umeme maana yake ni kuwa matumizi pia yanapanda!tunatumia umeme kupooza maji pamoja na vinywaji vingine,na siku hizi kila siku umeme unaisha kwahiyo hakuna jinsi zaidi ya kupandisha bei ya bidhaa la sivyo ni hasara tupu"alisema mmoja wa wafanyabiashara anaefanya biashara ya kuuza maji.

Nae Joice mathew mfanyabiashara wa salon ya kike akizungumza na muandishi alikiri kupanda kwa bei ya huduma hiyo na kusema kuwa zamani alikuwa akitoa shilingi 20000/- anapata unit 18 lakini kwa sasa ni unit 13 tu na hivyo njia pekee ya kulitatua hilo ni kuongeza bei ya huduma.

Kwa upande wao wananchi wamesema hawawalaumu wafanyabiashara kwa kuwa hawawezi kufanya biashara kwa hasara,bali wao wanailaumu serikali kwa kuto kuwajari na hivyo kuzidi kuwaongezea ugumu wa maisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni