Kurasa

Alhamisi, 23 Januari 2014

MBUNGE WA CHALINZE KUZIKWA IJUMAA.

Mazishi ya mbunge wa jimbo la Chalinze mh.Said Bwanamdogo aliefariki siku ya jumatano katika hospitari ya mifupa MOI jijini Dar es salaam yatafanyika siku ya ijumaa tar 23/01/2014.

Akithibitisha taarifa hizo mmoja wa ndugu wa karibu wa marehemu Bwanamdogo alisema kuwa ndugu wameamua maziko hayo yafanyike ijumaa kwa kuwa taratibu zote zitakuwa zimekamilika.

Viongozi kadhaa wanatarajiwa kuhudhuria katika mazishi hayo akiwemo mheshimiwa makamo wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine wa serikali.


Mheshimiwa Bwanamdogo atazikwa kijijini kwao miono siku hiyo ya ijumaa ambapo waombolezaji wakiwemo ndugu jamaa na marafiki wanatarajiwa kumsindikiza ndugu yao huyo mpendwa.Mungu ailaze roho ya marehemu mahari pema peponi.Amen

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni