visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Ijumaa, 18 Aprili 2014

KAMA UNATAKA KUSOMA DIPLOMA YA UALIMU SOMA TANGAZO HILI LA WIZARA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu:022-2110146/2110150/2/211679 Faksi:022-2113271, Tovuti: www.moe.go.tz TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 UTANGULIZI Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni wale wenye ufaulu mzuri katika mitihani ya kidato cha NNE na SITA.

KAMA UNATAKA UALIMU ANGALIA TANGAZO HILI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2, 211679, Faksi: 022-2113271, Tovuti: www.moe.go.tz
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 UTANGULIZI

WANAUME WENYE NGUVU WAINGIA MSITUNI KUWASAKA WASICHANA WALIOTEKWA NA BOKO NIGERIA.

Maafisa wa usalama, wawindaji na walinzi wanaendelea kuwatafuta karibu wasichana 100 wa shule waliotekwa nyara kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wasichana hao walitekwa nyara na kundi la Boko Haram siku ya Jumatatu.
Jeshi limekana taarifa yake ya awali iliyosema kuwa wengi wa wasichana hao walikuwa wamefanikiwa kutoroka.
Karibu wasichana thelathini wameaminika kutoroka kutoka kwa watekaji wao lakini huenda wengine tisisini na tisa wakawa bado wanazuiliwa na wapiganaji hao.
Wengi wa wazazi wa wasichana hao pamoja na jamaa wengine, waliwasaka wasichana hao Ijumaa kutwa katika msitu hatari wa Sambisa.
Mmoja wa wazazi wa wasichana hao, alisema msitu huo sio mahala salama pa kulala na hivyo walilazimika kuondoka.
Aliambia BBC kuwa aliona mahala ambapo panaonekana kama kambi ya wapiganaji wa Boko Haram ambao hawaishi tena msituni humo.
Kulikuwa na magari pamoja na pikipiki na kisima cha maji lakini watu waliokutana nao msituni walisema kuwa hawana habari kuhusu wasichana waliotekwa nyara.
Haijulikani idadi kamili ya wasichana waliotekwa nyara. Maafisa wanasema 99 hawajulikani waliko lakini wazazi wanasema kati ya wasichana 150 na 200 bado hawajapatikana

JARIBU MBINU HIZI ZA KIUCHUMI UNAWEZA KUTOKA.

1. Anza kuweka akiba ya T.Shs 1,000 kila siku. Tengeneza kisanduku na tumbukiza TShs. 1,000 kila siku. Zikifika TShs. 50,000 kafungue akaunti ya TAJIRIKA, kwenye Benki ya “
Standard Chatered”. Kisha endelea kuweka TShs. 30,000 kila mwezi. Jinsi mapato yako yatakavyokuwa yanaongezeka tenga asilimia kumi (10%) ya mapato yako uweke akiba kila
mwezi. Lengo lako liwe ni kuweka TShs 10,000 au zaidi kila mwezi. Fedha unayoweka ni kama unapanda mbegu. Kumbuka hii ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye utajiri. Faida katika
benki hii ni kubwa. Inaanzia asilimia 6.5% kwa kianzio cha TShs. 50,000 hadi TShs. 5,000,000 na asilimia 10% kwa kiwango kinachozidi TShs. 10,000,000. Fedha utakazoziweka huko usiziguse mpaka ukiona zimekuwa nyingi ndipo utaamua na kupanga ukaziwekeze sehemu gani.
2. Jifunze pia mbinu za kutafuta fedha. Njia rahisi ni ya uhakika ya kukuwezesha kufanikiwa kiuchumi katika maisha ni kutafuta mshauri au mtaalamu anayejua mbinu za uongozi wa biashara ili akushauri vizuri juu ya yale unayonuia kutekeleza.
3. Inawezekana pia bado hujawa na biashara ya aina yoyote. Kama ndivyo anza kufanya utafiti kuona utafanya biashara gani. Mawazo ya biashara gani ufanye unaweza kuyapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. Kila mara hakikisha unatenga asilimia 10% ya mapato
yako na kuweka kwenye akaunti yako ya TAJIRIKA. Kumbuka kwamba kuwa na biashara yako ni siri ya pili ya kuelekea kwenye kupata utajiri. Kama unayo biashara yako unaweza kumtafuta mtaalamu wa biashara kuangalia jinsi unavyoweza kuiboresha au kuipanua.
4. Panga malengo ya muda wa mwaka mmoja miaka mitano na miaka ishirini ili kuhakikisha kwamba unajikomboa kiuchumi. Malengo yako makuu yawe ni:- kuwa na akiba ya fedha za kutosha katika akaunti yako , kuwa na biashara yako, na vitega uchumi vya aina tofauti ambavyo unaweza kuvisimamia vizuri.
5. Kama wewe ni mwajiriwa, kipimo chako cha mafanikio kiwe ni kujiuliza swali, kama utaacha kazi yako ya mshahara utaweza kuishi kwa kutumia kipato chako cha pembeni kwenye
biashara yako kwa muda gani? Mafanikio yako yatakuja pale utakapoweza kutumia kipato chako cha ziada bila kutegemea mshahara, na hapo ndipo unaweza kuacha kazi na kwenda kuimarisha biashara zako au kuendelea na kazi huku pia ukijiimarisha kibiashara.
6. Kama utafuata mpango wa namna hii na kujituma kwa juhudi na maarifa kwa muda wa miaka mitano (5) unaweza kuwa tajiri na maisha yako yanaweza kuwa mazuri.
Kwa hisani ya Mmasi.

MMEKIMBIA LAKINI VIKAO VITAENDELEA.

Licha ya baadhi ya wabunge wa Upinzani wa Bunge Maalum la Katiba kuamua kususia kuendelea kushiriki katika mjadala wa Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa ndani ya Bunge hilo Kundi kubwa la Wajumbe hao waliobaki wataendelea kuchapa kazi waliyotumwa na Wananchi bila ya kujali uwamuzi uliochukuliwa na wale walioamua kutoka nje ya mjadala huo.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mbunge wa Bunge hilo Maalum la Katiba Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kutembelea baadhi ya Mabanda ya Maonyesho katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Dar es salaam ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kutimia Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Mwaka 1964.
Balozi Seif alisema Kundi hilo lililobakia ndani ya Bunge hilo halitatetereka kamwe na litatekeleza wajibu wake na lina uwezo kamili wa kukamilisha kazi hiyo kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Bunge hilo Maalum la Katiba na baadaye kuipeleka kwa Wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameelezea masikitiko yake na kuvunjwa moyo kutokana na kitendo hicho kilichoibuka ndani ya Bunge hilo ambacho hakionyeshi uungwana wala uvumilivu na kinaonyesha muelekeo wa kuwanyima haki ya Kidemokrasia Watanzania.
“ Kundi lililobakia ndani ya Bunge Maalum la Katiba ni kubwa na lina uwezo wa kutekeleza kazi hiyo muhimu katika Historia ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zetu tulizojipangia kwa pamoja sisi na wale walioamua kuukimbia mjadala huo “. Alifafanua Balozi Seif.
Akizungumzia suala la Muungano wa Tanzania kutimia miaka 50 tokea kuasisiwa kwake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Muungano huo umeleta faida kubwa kiasi kwamba Watanzania walio wengi wamenufaika nao Kiuchumi na Ustawi wa Jamii.
Alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeongeza kuleta upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi wa pande zote mbili na kuupa fursa kubwa zaidi Zanzibar katika kupanua wigo wa Kibiashara sambamba na umiliki wa maeneo makubwa ya ardhi kwa Wazanzibari walio wengi ambao kwa muda mrefu hivi sasa wanaendelea kuishi upande wa Tanzania Bara.
Balozi Seif alitanabahisha kwamba kwa vile Muungano wa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara ni wa asili ni vyema kwa watu wa pande hizo mbili wakaendelea kuuenzi na kuuimarisha kwa faida ya vizazi vya sasa na vile vijavyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Uongozi ulioandaa na kusimamia Maonyeso hayo ya kutimia Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa juhudi kubwa walizochukuwa na hatimae kufanikisha vizuri Maonyesho hayo.
Alisema Maonyesho hayo yamependeza kiasi kwamba wananchi wengi wamevutiwa nayo na kushawishika kutembelea kwa lengo la kujifunza na kuona bidhaa na harakati za kiutendaji za Taasisi na Mashirika ya Sekta za Muungano yaliyoamua kushiriki kwenye Maonyesho hayo.
“ Maonyesho ni mazuri na yamependeza. Ukweli nimefarajika na maandalizi ya Maonyesho hayo yenye kuonyesha maendeleo makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka 50 katika Taasisi na Mashirika ya Sekta mbali mbali za Muungano zinazofanya kazi Zanzibar na Tanzania Bara“. Alifafanua Balozi Seif. Balozi Seif aliwaomba Wananchi mbali mbali Nchini kuangalia Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupitia Maonyesho hayo ili wapate fursa kamili ya kujifunza kwa undani Historia hiyo.
Alisema hatua hiyo muhimu itasaidia kuwapa nafasi nzuri ya kuelewa ukweli na kujiepusha na watu na makundi yenye tabia ya kuendelea kuupotosha umma juu ya historia halisi ya Muungano huo unaoendelea kuwa kielelezo kikubwa katika Nyanja za Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifuatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa { TAMISEMI } Nd. Zubeir Sarataba alipata wasaa wa kutembelea baadhi ya Mabanda yaliyoshiriki kwenye Maonyesho hayo. Miongoni mwa Mabanda hayo ni pamoja na lile la Nguvu za Atomiki,Ofisi ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na Mambo ya Nje na Ushirikiano na Kimataifa. Mengine ni Banda la Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Kodi ya Ongezeko la thamani { TRA } pamoja na Banda la Mahakama ya Tanzania ambapo alibahatika kujionea hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na Taasisi hizo kupitia maonyesho hayo. Jumla ya Mabanda 50 ya Mashirika na Taasisi mbali mbali za Sekta za Muungano zinazofanya kazi pande zote mbili za Muungano Bara na Zanzibar zimeshikiri kwenye Maonyesho hayo ya kutimia Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Mwaka 1964.

WABUNGE WALIOSUSIA VIKAO WAFUTIWA POSHO NA WIZARA YA FEDHA.

Wizara ya Fedha kupitia Naibu wake Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba wametangaza uamuzi wa kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya mchakato wa Katiba vinavyoendelea Dodoma.
Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka matusi na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu April 10 20014 baada ya Waziri wa Fedha kupata safari ya kikazi nchini Marekani,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato huo wa Katiba.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza Benki zote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance ambazo zilipelekwa Bungeni April 16 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka April 30.
Uhakika wa taarifa hizi anazisema

BEI ZA MECHI YA SIMBA NA YANGA.

ANGALIZO TOKA TFF - KIINGILIO CHA CHINI YANGA vs SIMBA NI 7,000/-
Taarifa yetu tuliyotuma hivi punde ilionesha kiingilio cha chini mechi ya Yanga na Simba ni sh. 5,000.
Usahihi ni kuwa kiingilio hicho ni sh. 7,000 kama kinavyooneshwa kwenye tiketi.