Thursday, April 17, 2014
JK AFANYA UTEUZI WA MABALOZI KUJAZA NAFASI ZILIZO WAZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na Mabalozi wastaafu kwa mujibu wa sheria.
Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:
[image]
1. Balozi Dora Mmari Msechu (kushioto); ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stockholm, Sweden. Hadi uteuzi huu unafanyika Balozi Dora Mmari Msechu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anachukua nafasi ya Balozi Mohamed M .H. Mzale ambaye amestaafu.
Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moscow, Urusi. Hadi uteuzi huu unafanyika, Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba alikuwa Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Anachukua nafasi ya Balozi Jaka Mwambi.
[image]3. Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Joseph Edward Sokoine (kushoto) kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kabla ya uteuzi huu, Bw. Sokoine alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Ottawa, Canada.
Umetolewa na:
(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE
NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.
KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Alhamisi, 17 Aprili 2014
TWENDE KWA PILATO!
Thursday, April 17, 2014
KAIMU MKURUGENZI TANESCO KIZIMBANI KWA MATUMIZI MABAYA YA OFISI
Na Miriam Mosses
Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Semtutu na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh.milioni 200.
Washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Afisa Ugavi wa Tanesco, Hanin Mahambo, Mkurugenzi wa fedha Lusekeo Kasanga,Mwanasheria Godson Ezekiel pamoja na Mkandarasi Martin Abraham.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isidori Kyando alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa hayo katika tarehe tofauti mwaka 2011.
Kyando alidai kuwa shitaka la kwanza ni la matumizi mabaya ya Madaraka, Desemba 2011,katika ofisi za Tanesco Ubungo, jijini Dar es Salaam washtakiwa kwa pamoja walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji M/S Young Dong Electronic Co Ltd bila kuhakikisha kwamba Mkandarasi anafika katika kituo cha mwisho. Ilidaiwa kuwa washtakiwa walifanya kosa hilo kinyume na kifungu namba 35 (21) cha sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004 na kusababisha Martin Abraham kupata faida kutokana na ukandarasi huo. Katika shitaka la pili ni la kuisababishia serikali hasara linalowakabili mshtakiwa Semtutu, Mahombo,Kasanga na Ezekiel ambao wanadaiwa kwamba kati ya Januari hadi Desemba 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo waliisababishia serikali hasara ya Sh.275,040,000 kutokana na matumizi yao mabaya ya madaraka.
Washtakiwa wote walikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa mashitaka ulidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine ya kuwasomea washitakiwa hao maelezo ya awali.
Hakimu aliwaeleza washitakiwa hao kwamba dhamana yao iko wazi ikiwa watajidhamini wenyewe kwa kuwasilisha mahakamani hapo fedha taslim Sh.milioni 27.5 au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika.
Pia wawe na wadhamini wawili kila mmoja watakaoweka ahadi ya dhamana ya kiasi icho cha fedha.
Hata hivyo wadhamini hao hawakutimiza masharti na wamerudishwa rumande hadi Aprili 30, mwaka huu.

KESI YA PINDA YAPIGWA TAREHE.
Thursday, April 17, 2014
MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepiga kalenda kutoa uamuzi wa kesi ya kikatiba dhidi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hadi Mei 19 mwaka huu, itakapotoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na upande wa Jamhuri.
Uamuzi huo ulipangwa kutolewa jana lakini iliahirishwa mbele ya Msajiri Benedicto Mwingwa baada ya jopo linalosikiliza kesi hiyo kuwa bado halijamaliza kuandika uamuzi huo.
Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji waatu likiongozwa na mwenyekiti wao Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu.
Kesi hiyo Namba 24 ya 2013 ilifunguliwa na Kituo Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
LHRC na TLS,wanadai Pinda alivunja Katiba kutokana na kauli aliyowahi kuitoa bungeni wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji wa Sheria kuwapiga wananchi, wakati wa vurugu. Hivyo wanaiomba mahakama, pamoja na mambo mengine, itamke kuwa kauli hiyo ni kinyume cha Katiba na imwamuru Pinda aifute hadharani.

Hapa
Thursday, April 17, 2014
jeshi la polisi latahadharisha wananchi kuwa makini wakati wa sikukuu ya pasaka
SSP ADVERA SENSO
Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala la usalama wa maisha na mali zao.
Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na endapo vitajitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka.
Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Vilevile, Jeshi la Polisi linawataka madereva na watu wote watakaokuwa wakitumia barabara, kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka kwenda mwendo kasi, kujaza abiria kupita kiasi na kutumia vilevi wawapo kazini.
Wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi.
Aidha, wazazi wawe makini na watoto wao, kutokuwaacha watembee peke yao ama kwenda disko toto bila kuwa chini ya uangalizi wa watu wazima ili kuepusha ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.
Wananchi wakumbuke kutokuacha makazi yao bila uangalizi na endapo italazimu kufanya hivyo watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya, watoe taarifa haraka kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu yao, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.
Mwisho, Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya biashara hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, mahoteli na maeneo ya benki.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji wa wahalifu hao endapo uhalifu unatokea.
Tunawatakia Watanzania wote Pasaka njema.
Imetolewa na:- Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Jumatano, 16 Aprili 2014
HII NI MPYA YA MUDA HUU HUU KUTOKA MBEYA.
BREAKING NEWS JESHI LA POLISI JIJINI MBEYA LIMELAZIMIKA KUTUMIA NGUVU ZA ZIADA KUWASAMBARATISHA WAMACHINGA AMBAYO WAME KOSA ENEO KUFANYA SHUGHULI ZAO, SEHEMU RASMI LA SERIKALI KWA AJIRI YA SHUGHULI HIZO HAZIFAI, WANADAI POLISI WAME LAZIMIKA KUWA RUSHIA MABOMU YA MACHOZI... ASEMA COMMANDA WA KIKOSI CHA POLISI JIJINI MBEYA
HUKU VIJIJINI HALI NDIO TETE KABISA
BASI LA ABIRIA LIKISAFIRI KATIKA NJIA YA TOPE KUTOKA HANDENI KWENDA JIMBO LA MUHESHIMIWA BEATRICE SHELUKINDO KILINDI, LIKIWA LINAJITAHIDI KWENYE TOPE KUWAFIKISHA ABIRIA HAO NYUMBANI.SERIKALI NA HUKU PIA WANALIPA KODI!, MUWAKUMBUKE SIO KWENDA KUFUNGA VIBANDA VYAO TU WAKATI WA KUKUSANYA KODI, BILA KUWAPA HUDUMA STAHIKI.
DA!KITIMOTO BANAAAAA
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.
Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.
Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.
Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.
“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii.
“Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema Profesa Lekule.
Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.
Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.
Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.
Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.
“Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika,” alibainisha Profesa Lekule

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)