Kurasa

Ijumaa, 22 Aprili 2016

UONGOZI KATIKA BIASHARA #BUSINESS MANAGEMENT#


PICHA(Bing.com);Uongozi sio ukali
.
Hujambo mpenzi msomaji mtu wangu wa kazi na karibu tena katika mfululizo wa mada zetu hizi ambazo kwa kipengele hiki tunamalizia kabla ya kuanza kukuletea upande wa pili ambapo tutakuwa tunaangalia biashara mbalimbali na fulsa nchini Tanzania. Tutaangalia mitaji yake ya kuanzia,faida zake,changamoto zake na hasara zake.Cha msingi ni wewe kuwa msomaji namba moja wa chombo hiki cha habari na kuendelea kufuatilia kila siku bila kukosa. Ni wakati mwingine tena ambapo Tunamshukuru mwenyezi MUNGU kwa kuendelea kutupatia pumzi yake.

Leo katika mada hii tutaangalia uongozi katika Biashara yako na unapaswa kunifuatilia kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Kama utakuwa na swali au maoni tafadhali andika hapo chini baada ya kusoma mada hii nami nitakujibu wakati huohuo.Tutahakikisha kila comment inayoandikwa hapa inajibiwa ipasavyo.TUENDELEE..


Biashara yako inaweza kukua kiasi ambacho unaweza kuhitaji wafanyakazi kwaajili ya kukusaidia.Kuajiri wafanyakazi kunamaana kuwa utapaswa kuwa kiongozi wa wengine.Ingawa unapaswa kuwa kiongozi wa biashara yako hata kabla  ya kuajiri watu,Kuongoza watu ni tofauti na kujiongoza mwenyewe.Hapa unacheza na hisisa za watu.Unapaswa kuwa na mambo mathubuti ili kuepuka kuivuruga biashara yako kutokana na makosa ya kiuongozi.

Moja kati ya waandishi wa maswala ya uongozi bwana MARX WEBER aliorodhesha mambo sita ambayo watu wengi huyatumia kuendesha biashara na taasisi zao.Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na;

>>MGAWANYO SAHIHI WA MAJUKUMU<<
Majukumu ni lazima yagawanywe kulingana na uwezo wa mtu katika kitengo husika na kuwe na uwiano sahihi kati ya madaraka na majukumu.

Katika mgawanyo huo wa majukumu hakupaswi kuwa na kuingiliana kimajukumu kati ya secta moja na nyingine.Kila mfanya kazi anapaswa kuwa huru kufanya yale yanayompasa kufanya.

Takwimu zinaonesha kuwa watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi.Hii inatokana na kupoteza kujiamini kutokana na kuingiliwa majukumu katika kazi au kiutendaji.Upande mwingine ni kwa watu wengi kuacha kazi na kutafuta kazi mahali pengine kutokana na kuepuka mabosi wa aina hii.Kwa hiyo unaweza pia kupoteza wafanyakazi mala kwa mala.

Dada mmoja ambae alikuwa mfanyabiashara wa ''chipsi mayai'' alifanikiwa kuiendesha biashara yake vizuri sana akiwa peke yake mpaka ikafikia kipindi ambacho biashara ilikuwa kubwa kiasi kwamba asingeweza tena kufanya peke yake kutokana na wingi wa kazi pamoja na wingi wa wateja.Kutokana na hali hiyo dada yule sasa alihitaji kuajili wafanyakazi wa kumsaidia kazi.

Dada yule aliajiri wafanyakazi watatu.Wawili aliwapa kazi ya kuuza wakati mmoja alimtumia kumenya viazi kuchota maji na kufanya kazi nyingine za usafi.

Biashara ilifanikiwa sana na mapato yake yalipanda maradufu mala mbili ya mwanzo.Kwa bahati mbaya dada yule hakuwa mvumilivu kwa makosa madogo madogo yaliyokuwa yanafanywa na wafanyakazi wake ambayo pengine angepaswa kuongea nao na kuwaelekeza kwa utaratibu.Alikuwa na ''mdomo mchafu'' sana kwa wafanyakazi wake.

Pamoja na mapato ya biashara kupanda asilimia kubwa ikiwa imechangiwa na wafanyakazi wale,ndani ya miezi mitatu tu wafanyakazi wote watatu waliacha kazi.Kuanzia wakati huo dada yule alikuwa kila akiajiri wafanyakazi wanamkimbia.Ilifikia wakati wafanyakazi wapya walikataa kufanya kazi mahali hapo na hatimae ilimbidi aendelee kufanya kazi peke yake na hatimae ilimshinda.Tafakari.

>>MTIRIRIKO WA MAAGIZO<<

PICHA(Bing.com);Mpe uhuru mfanyakazi wako.

Kama biashara ni kubwa kiasi cha kuwa na wafanyakazi wengi ambapo kunakuwa na mpangilio wa majukumu kutoka ngazi ya juu kabisa mpaka chini kabisa,ni vizuri pia mtiririko wa maaagizo ukaenda katika mfumo huo.Agizo likitoka kwenye uongozi wa juu linapaswa kufuata vitengo vyote ambavyo maagizo yanapita mpaka kumfikia mhusika.

Mfano,kama biashara imekuwa kiasi cha kusajiriwa kama kampuni mkurugenzi unapaswa kumpa maagizo meneja ambae atatoa maagizo kwa wafanyakazi wengine kulingana na nyazifa zao.

>>SHERIA NA MIONGOZO<<
Lazima kama kiongozi katika biashara yako utengeneze sheria,miongozo na kanuni pengine kwa kuwashirikisha wafanyakazi wengine.Sheria hizi zitakusaidia sana wakati wa kufanya maamuzi pale inapobidi kufanya hivyo na hivyo kupunguza malalamiko kutoka kwa wale wanaofanyiwa maamuzi hayo.

Kufanya kazi na watu bila sheria ni sawa na kumruhusu kila mmoja kufanya kulingana na matakwa yake binafsi na hatimae ni kuivuruga biashara yako kwasababu inaweza kupoteza kuaminiwa kutoka kwenye soko unalolitegemea.

Pamoja na sheria ni vizuri pia kuwa na mikataba kwaajili ya wafanyakazi wako.Mikataba ni kitu muhimu kwasababu huwa inatoa haki kwa pande zote mbili,muajiriwa na mfanya kazi

Asante sana mpendwa msomaji na mtu wangu wa kazi kwa kunifuatilia kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Usikose kuendelea kufuatilia katika mafunzo yetu mengi ambayo yanaendelea kukujia kila wakati.

Usisite kutoa maoni yako hapo chini au kuuliza maswali kama yapo na utajibiwa wakati huohuo.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni