Kurasa

Jumatatu, 25 Aprili 2016

TAZAMA SAMAKI ALIEVULIWA NA HUYU JAMAA.(PICHA)

PICHA; SAMAKI AINA YA OAR ALIEVULIWA HUKO TAIWAN.

Mvuvi mmoja huko Taiwani alifanikiwa kumvua samaki mkubwa aina ya OAR aliekuwa na urefu wa mita tano.Kwa mujibu wa wataalamu,samaki huyo alievuliwa alikuwa ni mtoto kwasababu aina hiyo ya samaki huwa wanakuwa wakubwa kufikia kiwango cha urefu wa mita 1000 na ni mala chache sana kufanikiwa kuwavua samaki hao kwasababu wanakaa kwenye kina kirefu sana cha bahari.



PICHA;MVUVI AKITENGENEZA WINDO LAKE.

Inaaminika kuwa samaki huyo mkubwa alisogea maeneo hayo ya pembezoni mwa bahari kwa sababu ya kuogopa matetemeko mawili yaliyotokea hivi karibuni huko Taiwani.

Kutokana na ukubwa wa samaki huyo mvuvi aliemvua alipiga picha na samaki huyo akionesha jinsi anavyomchangua na kuipost kwenye mitandao ya kijamii kabla hajamfaidi samaki huyo na familia yake.

PICHA;MTOTO AKISHUHUDIA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni