Kurasa

Jumapili, 17 Aprili 2016

TABIA BINAFSI/HULKA NA ATHARI ZAKE KATIKA BIASHARA. #PERSONALITY AND ITS BUSINESS EFFECTS#

PICHA(Photobucket.com);OPRAH WINFRED.mwanamke aliefanikiwa duniani.

Umewahi kutafakari jinsi unavyojichukulia na jinsi unavyotaka watu au jamii ikuchukulie.Tambua kuwa mala nyingi jamii hupenda kufanya au kukufanyia vile unavyojifanyia mwenyewe.



Watu wengi wameshindwa kwenye kipengele hiki.Wanafanya biashara au mambo mengine ya kimaendeleo lakini ndani ya nafsi zao wanakuwa wameshakiri kuwa hawaliwezi jambo wanalofanya na matokeo yake ni kushindwa kweli kufanya jambo hilo.
Umewahi kujiuliza,kwanini mtu anasoma miaka mingi halafu anaajiliwa au anakosa ajira kwa interview ya siku moja tu?Hii ni kwasababu lengo la Interview ni kuangalia kama mhusika anakiri na kuamini kwamba anaweza,anaipenda na atakuwa huru kuifanya kazi anayohitaji kupewa.Wahusika kimsingi huwa hawasikilizi sana maneno ya muombaji wa ajira bali huangalia matendo yake ambayo huwakilisha kile anachokiongea kwa ndani.
Mfanyabiashara na mwingine yeyote unapaswa kujua binadamu hana ''mdomo'' mmoja.Hii maana yake ni kuwa kabla ya kutamka maneno mdomoni binadamu huwa tunazungumza ndani ya nafsi zetu.Maneno hayo tunayozungumza ndani huweza kuonekana nje hata kama tumekaa kimya mdomoni.
Jijengee tabia ambazo zitakuwekea mazingira mazuri kibiashara au mafanikio kuanzania ndani.Mtu hazaliwi na kujiamini lakiini anaweza kujifunza kujiamini.Ili kujifunza kujiamini kwanza tuangalie mambo ambayo humuondolea mtu kujiamini;
i)Kufanyiwa ukatili tangu utotoni kama vile kubakwa,kupigwa mala kwa mala,kufokewa ovyo,kukeketwa,ndoa za utotoni na mengine mengi.
ii)Uchafu
iii)Upweke
iv)Uhalifu nakuvunja sheria
v)Kuhisi kukosa uwezo fulani.

i)Kufanyiwa Ukatili.
Hili ni moja kati ya mambo sugu ambayo huwasababishia watu wengi sana tabiua ya kujiamini.Kwa bahati mbaya ukatili mala nyingi hufanywa na ndugu jamaa na marafiki zetu wa karibu.Wakati mwingine jamii au mtu mmoja mmoja hujikuta wakifanya ukatili kutokana na mifumo yetu ya kimaisha.Kwa mfano jamii ya wamasai zamani ilikuwa na utamaduni wa ndoa za utotoni na hivyo kupelea wanawake katika jamii hizo kupoteza kujiamini na kuamini kuwa wao ni vyombo vya wanaume.

ii)Uchafu.
Hii ni tabia ambayo mtu huitengeneza taratibu kuanzia utotoni au ukubwani.Kwa bahati mbaya mtu huweza kuwa mchafu na akajua kwamba ni mchafu na wakati huohuo anakiri kwamba jamii haipendi uchafu.Kutokana na kuujua ukweli huo mtu huyo anapokuwa katika jamii husika hujikuta akitumia muda mwingi kujifikiria yeye mwenyewe,alivyo mchafu na jamii inavyomchukulia kwa wakati huo na mwisho wa siku hupoteza kujiamini na kushindwa kutenda kile kinachompasa kufanya.

iii)Matabaka. 
Dunia tunayishi sasa imejengwa na matabaka,na huu ni ukweli ambao hauwezi kupingika au kibadilishwa.Hii ni kwasababu hata asili ya ngozi zetu na maumbile yetu binadamu pengine na viumbe wengine kuna matabaka.
Kiuhalisia matabaka sio jambo baya na ndio linalopendezesha dunia.Ukkiangalia wahindi na asili zao ni tofauti na waarabu na waafrika,watoto wadogo ni tofauti na watu wazima,vivyo hivyo kwa wanawake na wanaume.
Kumbuka kuwa kwa kutumia tofauti zetu tulizonazo ndio kwa pamoja tunaweza kufanya kitu ambacho pengine kisingeweza kufanyika kama tungefanana.Watu wasiojiamini kutokana na kipengele hiki ni wale wanaoamini kuwa wakiwa na kundi fulani hususani wasomi yeye hawezi kufanya kitu.
l
PICHA(nailaland.com);LINDA IKEJI(Kulia).Blogger aliefanikiwa Afrika na duniani kwa jumla.

iv)Upweke.
Huu huweza kuleta kutokujiamini pale ambapo muda mwingi mtu hujitenga na kukaa mazingira ya peke yake.Mtu wa iana hii anapokuwa kwenye kundi la watu wengi hupoteza kujiamini na kujiikuta anashindwa kuwasilisha kile kinachomhusu.

v)Uhalifu wa kuvunja sheria.
Bahati mbaya ni kuwa mtu anaweza kufanya tukio la kihalifu lakini nafsi yake ikawa haikubaliani na swala hilo.Kutokana na hilo nafsi ya mtu huyo hutengeneza hali ya woga na kuamini kuwa sehemu yoyote yenye watu anaweza kufahamika na kukamatwa.Hii humtengenezea mhalifu hali ya kutokujiamini anapokuwa na watu na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake.

vii)Kujiumbia hisia za udhaifu zisizo halisi.
Kumekuwa na hali ya watu kujitengenezea mazingira magumu ndani ya nafsi zao ya kufanya kazi wanazozifanya kuwa ni ngumua au haziwezekani.Hili linapokuja katika uhalisian hata kama ni kazi rahisi mtu hujikuta anaishindwa kwa kuwa alishajenga mazingira ya ugumu ndani ya nafsi yake.

NINI CHA KUFANYA.........
Kama nilivyotangulia kusema awali,kama unatabia ya kutokujiamini,huyu ni adui mkubwa sana wa maendeleo yako binafsi na jamii kwa ujumla.Unapaswa kuchukua hatua kumdhibiti adui huyu kabla halijawa tatizo kubwa.

i)Jisahaulishe ya nyuma.
Siku zote katika maisha unapaswa kujua kuwa jana imepitya na haitarudi tena.Epuka kupoteza muda mwingi ukiwaza yale yaliyokutokea siku za nyuma.Pia unaweza kuwaepuka watu waliokufanyia ukatili au wanao kufanyia ukatili na kusababisha hali ya kutokujiamini.
Mfano wa watu maarufu waliokiri kufanyiwa ukatili lakini wakasahau na kusongo mbele ni mwanadada ambae kwa sasa yupo kwenye orodha ya wanawake matajiri duniani Oprah Winfred na Blogger maarufu duniani Linda Ikeji.

ii)Kuwa nadhifu.
Bila kujali unafanya kazi gani,jitahidi sana kuwa msafi na nadhifu.Unapokuwa nadhifu inakutengenezea tabia ya kutaka watu wakuone wewe na kile unachokifanya na hii hukujengea kujiamini sana hususani unapokuwa mbele za watu.
Pia unadhifu unaweza kukutengenezea fulsa nyingi sana za kazi na biashara.
Kuna tabia ipo mitaani ambapo unapomuuliza mtu kwanini anakuwa mchafu,jibu linalotoka huwa ni kwasababu ya umaskini.Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya umaskini na tabia ya uchafu.
Nimeshawahi kushuhudia mtu mmoja akiwa na nguo za aina moja tu na kila siku akiwa msafi kabisa na nadhifu.
KUMBUKA.Unapokuwa mchafu unazidi kufanya maisha yako kuwa ''machafu'' pia.

iii)Badilisha mtazamo kuhusu matabaka.
Unapaswa kujua kuwa katika kila kundi kwenye jamii kuna kitu tofauti ambacho kundi jingine halina na lingependa kukipata kitu hicho.Kwa mfano watoto wadogo ambao ni mfano halisi wa tabaka la chini huweza kumpa fulaha mzazi au mtu yoyote anapotoka kazini na hivyo kumuondolea stress au kumsahaulisha na magumu ya kazi ya kutwa nzima.Hoo maana yake ni kuwa watoto wanamiliki kitu ambacho ni faraja kwa wakubwa.Kutokana na mfano huo mtoto ni mtu muhimu sana kwenye jamii kama alivyo mtu mzima.

Vivyo hivyo kwa madaraja na matabaka mengine,kuna kitu ambacho mtu mweusi anacho ambacho mtu mweupe hana na anakihitaji.Kuna kitu fulani anacho mlemavu ambacho watu wengine hawana na wangependa kuwa nacho.Mfano wa hili ni msanii Keisha wa Tanzania ambae ana uwezo mkubwa wa kuimba na amekionesha kipaji chake bila kujali alivyo na mwisho wa siku amefanikiwa wakati huohuo kuna mamia ya wasanii Tanzania ambao wanajitahidi kumfikia Keisha lakini hali ni tete.

iv)Jichanganye na watu.
Ukiachilia mbali kujiamini moja kati ya njia zinazoweza kukusaidia kupata mafanikio ni pamoja na kujichanganya na watu.Mfanyabiashara au mtu yeyote anaetaka kuwa mjasiriamali anapaswa kukaa na wajasiriamali au wafanyabiashara wakubwa na kupata ABC za biashara.Wazungu husema ''The bird with the same feathers froke together.Tengeneza kujiamini kwa kujichanganya na watu waliofanikiwa na kuchangia mada panapostahili ili kujitengenezea mtandao na imani kwa wafanyabiashara wenzako na wewe mwenyewe.

v)Hudhuria Ibada.
Kama uliwahi kufanya uhalifu fulani katika maisha yako(kubaka,kuiba,nk) na unahisi inakusababishia hali ya kutokujiamini,jitahidi ujiunge na dini mojawapo ya zilizopo na uhudhulie ibada.Hii itakusaidia kutubu dhambi na makoso yako kwa MUNGU kitu ambacho kinaweza kuifanya nafsi yako kuamini imesamehewa na hivyo kukurudishia kujiamini.Unaweza pia kumtendea jambo jema mtu uliewahi kumfanyia uhalifu pamoja na kumuomba msamaha hata kama utaficha utambulisho wako.Akionesha dalili yoyote ya kukusamehe basi itakuwa hatua kubwa sana katika maisha yako.

##Muamini aliekuumba##.
Siku zote unapaswa kuamini kuwa aliekuumba alikuwa na kusudio maalum la kukuleta duniani.Hakuna mtu alieletwa duniani kuangalia tu wenzake wakijenga maghorofa makubwa na kutengeneza magari halafu baada ya hapo afe.Kila mtu ameumbwa kwa kazi maalum na ni kazi ya mtu binafsi kutambua ameumbwa na nini na anapaswa kufanya nini.

Mpenzi msomaji leo tumefika mwisho wa mada yetu ambayo ni mfululizo wa mada zetu zinazopatikana katika kitabu changu cha MIMI NI TAJIRI kinachouzwa mtandaoni.Endelea kufuatilia mfululizo wa mada hizi mala kwa mala zinapotoka ili upate maalifa haya ambayo yatakusaidia sana katika safari yako ya mafanikio.Usisahau kusoma mada za jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo chaki na sabuni zote ili ujitengenezee vitu hivyo nyumbani kwako na kuuzia watu hatimae ufanikiwe kama watu wengine.Unaweza pia kuwasiliana nami kwa njia ya ujumbe tu katika 0654627227,tafadhari usipige namba hii kwasababu haitapokelewa lakini ukituma ujumbe utajibiwa hapohapo.ASANTE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni