Kurasa

Alhamisi, 28 Aprili 2016

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI UNABUNI JINA LA BIASHARA YAKO.

business: Portrait thinking handsome man looking up with idea light bulb above head isolated on gray wall background
PICHA;FIKIRIA KWA MAKINI KUHUSU JINA LA BIASHARA YAKO.

Wafanyabiashara wamekuwa wakichukulia jina la biashara kama kitu cha kawaida na sio moja kati ya vipaumbele katika mambo yao muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara.Kufanya hivyo ni makosa kimsingi kwa sababu huweza kuleta madhara makubwa katika biashara yako hususani wateja wako wanapokutana na wateja wapya wanaohitaji kuijua biashara yako.


Wakati unapoanzisha biashara yako jina ni jambo muhimu sana la kuzingatia.Pamoja na kuwa jina lina umuhimu lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kufanya jina la biashara yako kuleta matunda unayoyakusudia.Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo mfanyabiashara unapaswa kuzingatia wakati unabuni jina la biashara yako;

JINA LAZIMA LIWE FUPI.
Majina marefu ni rahisi sana kusahaulika na ni vigumu kuyakumbuka tena. Hakikisa jina la biashara yako linakuwa fupi na lenye kuvutia katika midomo ya watu.Ufupi wa jina unafanya iwe rahisi kulitamka na kulirudiarudia na hatimae kuzoea katika vichwa au midomo ya watu.Wakati unabuni majina jaribu majina matatu harafu ushirikishe wengine ni jina gani zuri kuliko mengine mawili.

LINALOAKISI KILE KINACHOFANYWA NA BIASHARA YAKO.
Jitahidi sana kubuni jina ambalo linapotamkwa akili ya mtu inampeleka katika aina fulani ya biashara.Hii ni muhimu sana hususani kwa wafanyabiashara ambao hawafahamiki na wanahitaji wateja kwaajili ya biashara zao.Jina la biashara linapoakisi biashara husika inakuwa rahisi kwa wateja kufahamu unachokiuza na hatimae kuanza kuipa biashara yako umaarufu.

LINALOGUSA HISIA ZA WATU.
Moja kati ya njia ya kupata wateja katika biashara yako ni kuipa jina ambalo linagusa hisia za watu.Kumbuka washindani wa biashara yako ni wengi na kila mmoja anafanya mbinu mbalimbali kuhakikisha wateja hawaendi kwenye biashara nyingine isipokuwa zao.Jitahidi kuzigusa hisia za watu wanapotamka jina la biashara yako ili kuwafanya waikumbuke wakati mwingine.Mfano badala ya kusema ''DUKA LA MAFUTA YA WATOTO'' Unaweza kuliita ''MTOTO SHOP''.

LIFANYE KUWA RAHISI.
Jina la biashara halitakiwi kuwa na misamiati migumu ambayo itamfanya mteja kupata shida anapohitaji kulikumbuka na kulitamka tena.Pamoja na urahisi huo bado jina linatakiwa kuwa na vigeza vinavyotakiwa.

LA KIPEKEE.
Hupaswi kunakiri majina ya biashara nyingine.Chagua jina la kipekee ambalo litakutambulisha wewe na biashara yako.Kuipa biashara yako jina la biashara nyingine inaweza kuleta athari kwa biashara yako kwani unaweza kuwa unaitangaza biashara  ya mtu mwingine bila kujifahamu hususani kama biashara ya mtu huyo imekuwa kubwa kuliko yako.

Tutumie maoni yako hapa chini kama kuna lolote unataka ku share na sisi.Pia kumbuka kushare ni kujari kile tunachokupatia.Bonyeza vitufe vya facebook na twitter vilivyoka hapo chini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni