Kurasa

Jumatano, 20 Aprili 2016

AFYA,JINSI YA KUILINDA NA UMUHIMU WAKE KATIKA BIASHARA #HEALTH,HOW TO PROTECT IT AND ITS IMPORTANCE IN BUSINESS#


PICHA(Bing.com); AFYA DHAIFU INAWEZA KUATHIRI KAZI ZAKO.

Uhali gani mpenzi msomaji na mpenda maendeleo ambae umekuwa ukijipa muda kidogo kupitia mitandao inayokuelimisha kama huu badala ya kupoteza muda tu kwenye mitandao ya kijamii.Karibu sana kwenye mfululizo wa mada zetu hizi na nina imani kubwa sana kuwa baada ya kusoma mada hii utakuwa umeongeza kitu katika benki yako ya mambo ambayo tayari umeshapitia kwenye mtandao huu na kuelimika.Kwa wale wageni hapa kumbuka kusoma mada nyingine zilizopita za kibiashara ambazo zitakupa mfululizo mzuri na hatimae unapojifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali utakuwa na ujuzi mkubwa wa kufanya biashara na Mungu atakubariki


Afya ni muhimu sana hususani katika maendeleo ya Biashara zetu.Kuna mambo ya kuzingatia ili kulinda afya zetu na kuepuka athari zinazoweza kutokana na biashara zetu kama ifuatavyo;

  • TUMIA VIFAA MAALUM KUJILINDA WEWE MWENYEWE.
Kuna aina za biashara ambazo ukifanya bila tahadhari kiafya unaweza kupata madhara makubwa baada ya muda mrefu au muda mfupi.Biashara kama kuuza cement,ufundi selemala.Kinyozi,Kuzoa uchafu manispaa za majiji na miji,Mama ntilie,Kilimo nk ni baadhi tu ya biashara ambazo mhusika au wahusika wanapaswa wao pamoja na wafanyakazi wao kutumia vifaa maalum kujikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na kazi hizo.Kwa mfano mkulima anapopiga dawa za kuua wadudu kwenye mazao yake anapaswa kuziba pua pamoja na mdomo wake asije na yeye kudhulika na dawa hizo.


Unatakiwa kujielimisha kuhusu biashara unayofanya,athari zake kiafya na jinsi unavyoweza kujikinga na athari hizo.Kujielimisha ni pamoja na kupata elimu kutoka kwa wataalamu wa afya wa sekta husika na kuchukua hataua kutokana na elimu hiyo.


  • WALINDE WATEJA WAKO.
Unapofanya biashara yoyote hakikisha kwa makini kabisa wateja wako wanakuwa salama.Epuka kuwaudhia wateja bidhaa ambazo zimekwisha muda wake au hazikuthibitishwa na mamlaka husika kama vile TBS ya Tanzania.


Kuna athari mbaya sana kwako na kwa biashara yako kama hutachukua hatua kuwalinda wateja wako.;

-Kwa upande wako binafsi kiama mfanyabiashara,usipowalinda wateja wako inaweza kukupelekea hata kupelekwa gelezani.Kwa mfano kama una duka la vyakula,lakini pia unauza na sumu za panya, ikatokea bahati mbaya sumu ya panya ikaingia kwenye chakula bila wewe kujua na hatimae mteja akatumia chakula hicho na kudhulika wewe ndio utawajibika kwa hilo.

-Pia biashara yako inaweza kudhurika endapo wateja wataambiana kuhusu kukosekana umakini katika biashara yako.Angalia mfano ufuatao;

Wakati fulani nilikuwa nafanya biashara mbali na nyumbani na hivyo ilinilazimu kula kwa mama ntilie.Nilikuwa nakula kwenye moja ya migahawa iliyokuwa karibu na biashara yangu na ilikuwa karibia kila siku lazima niende kula hapo.
Kwa bahati nzuri wafanyabiashara wengine wengi pia walikuwa wanakula katika mgahawa huo.Dada aliekuwa anamiliki na kuuza vyakula katika mgahawa ule alikuwa pia anamiliki salon ya kike na alikuwa akihudumia biashara zote mbili.
Siku moja jamaa mmoja aliekuwa anafahamika kwa jina la John ambae alikuwa mfanyabiashara wa nyama katika bucha lililokuwa karibu kabisa na biashara yangu alienda kujipatia chakula cha mchana katika mgahawa huo.
Wakati akiendelea kula ubwabwa uliopikwa vizuri,bahati mbaya alikutana na vywele ndani ya chakula hicho.Bwana John hakuwa mtu wa uvumilia mambo yanapomkera.Aliacha kula na kupasa sauti yake huku akimwambia kila mtu aliekuwa eneo hilo.
Kuanzia siku ile sikujisikia tena kula katika mgahawa ule na yule dada alipoteza wateja wengi sana kutokana na tukio lile.

  • PAMBANA NA STRESS KWA VITENDO
Biashara inaweza kukuletea stress nyingi sana ambazo zinaweza kufanya afya yako kudorora.Njia pekee inayoweza kukusaidia kupambana na stress za kiubiashara ni kutambua changamoto za biashara yako,Kufikiria sana kuhusiana na suluhisho la changamoto hizo au kutafuta mawazo kwa wafanyabiashara wenzio na kuzitatua changamoto hizo.
stressed people: Concept of stress with businessman with a rock on the head Stock Photo
PICHA;STRESS NI MZIGO.
  • EPUKA KUJIONEA HURUMA.
Watu wengi hufikiri kujionea huruma ndio njia muafaka wa kulinda afya zao.Hii kwa bahati mbaya ndio njia inayoongoza katika kujiangamiza.Unapojionea huruma inakuwa ngumu sana kufanya kazi na kupambana na magumu ya biashara.

Yesu,moja kati ya mitume au manabii wanaoongoza kuwa na wafuasi wengi katika ulimwengu huu aliwahi kuwaambia wafuasi wake sentensi hii ''Yeyote atakae kuiokoa nafsi yake ataiangamiza,na atakaekuiangamiza nafsi yake kwaajili yangu ataisalimisha'' Hapa ninaweza kuongeza kusema kuwa yeye atakaekuiokoa nafsi yake ataiangamiza na yeyote atakae kuiangamiza nafsi yake kwaajili yake na kwa familia yake ataisalimisha.

Maneno haya yanachukua nafasi ubwa sana kwenye maisha ya kawaida.Ni rahisi sana kufa na njaa kama hutatoka kushughulikia vikwazo vya kimaisha.Kutokana na kujionea huruma unaweza kujikuta unawaza sana kuhusu jinsi ya kupata pesa badala ya kwenda kutafuta pesa na hatimae ukaishia kuwa na ndoto za mchana na ku mlaumu Mungu kwamba anawapa wengine na wewe anakusahau.Kumbuka msemo usemao mkaa bure sio sawa na mtembea bure.

Mpenzi msomaji tukutane wakati mwingine katika muendelezo wa mada hizi ndefu lakini zinazokupa elimu ya kutosha kabisa katika biashara yako.Kama kuna lolote la kushare na mimi tuma ujumbe mfupi kwenye 0654627227 au unaweza kuandika maoni yako hapa chini baada ya kusoma mada hii na mimi nitakujibu hapa hapa.Kwa wale wanaotaka kuwasiliana kwa maswala ya kibiashara au matangazo tumia mdeonidas@gmail.com.

ASANTE.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni