Kurasa

Alhamisi, 25 Juni 2015

AAGA DUNIA SIKU TATU BAADA YA HARUSI




null

Kijana  mmoja aliefahamika kwa jina la Omar Al Shaikh (16) ameaga dunia ndani ya siku tatu kwa ugonjwa wa saratani ya damu unaofahamika kwa jina la Leukemi baada ya ndoa na mchumba.Kijana huyo alimuoa mpenzi wake aliefahamika kwa jina la Amie Cresswell (16) katika wodi ya hospital ya Malkia Elizabeth iliyoko Birmigham Uingereza.



Imefahamika kwamba kijana huyo aliaga dunia siku ya jumatatu baada ya kukosa mtu wa kumuongezea damu Kutokana na asili yake ya Kirumi na Kiarabu ilikuwa vigumu sana kupata mtu mwenye chembechembe zitakazoingiana.
Mamake alisema tangu afahamishwe kuhusu kuzoroteka kwa hali yake ya siha mapema mwezi huu Omar amejitahidi kuwa mchangamfu hadi alipoaga dunia.
''Aliaga dunia usingizini''alisema mama huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni