Kurasa

Ijumaa, 26 Juni 2015

MTU MMOJA AUAWA UFARANSA

Mtu mmoja amechinjwa na mwingine kujeruhiwa nchini Ufaransa na mvamizi mmoja aliekuwa akipeperusha kibendera cha kiislamu katika eneo lililofahamika kwa jina la Saint-Quentin-Fallavier.

Alhamisi, 25 Juni 2015

AAGA DUNIA SIKU TATU BAADA YA HARUSI




null

Kijana  mmoja aliefahamika kwa jina la Omar Al Shaikh (16) ameaga dunia ndani ya siku tatu kwa ugonjwa wa saratani ya damu unaofahamika kwa jina la Leukemi baada ya ndoa na mchumba.Kijana huyo alimuoa mpenzi wake aliefahamika kwa jina la Amie Cresswell (16) katika wodi ya hospital ya Malkia Elizabeth iliyoko Birmigham Uingereza.

Jumanne, 23 Juni 2015

MTU MBAYA KULIKO WOTE UGANDA APATA MTOTO

 
Godfrey Baguma, 47, mwanaume ambae anadaiwa kuwa ndio mwenye sura mbaya kuliko wote nchini Uganda amejipatia mtoto wake wa nane na mke wake wa pili anaefahamika kwa jina la, Kate Namanda mwenye umri wa miaka 30.Jamaa huyo amejipatia mtoto wa kike mapema wiki hii na ameonekana kufurahia sana ujio huo wa mtoto wake.

Jumanne, 16 Juni 2015

MORSE AHUKUMIWA KIFO

Mahakama ya juu ya Misri imehakiki hukumu ya mahakama ya chini ya kumnyonga rais wa zamani Muhammad Morsi kwa makosa ya kupanga njama ya kuwatorosha wafungwa katika kipindi cha maandamano ya kumng'oa madarakani rais aliyekuwepo Hosni Mubarak mwaka wa 2011.
Hukumu hiyo inafuatia majadiliano baina ya majaji wa mahakama kuu na kiongozi wa kidini Mufti.
Awali mahakama ya chini ilikuwa imemhukumu kifungo cha maisha Morsi, kwa kosa la kufanyia ujasusi kundi la Kipalestina la Hamas, kundi la wapiganaji la Hezbolah na Iran.
Viongozi wengine 16 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood , akiwemo kiongozi wao Khairat el Shater,walihukumiwa kifo.
Bwana Morsi pia anakabiliwa na hukumu tofauti ya kifo baada ya kupatikana na kosa la kushiriki katika kupanga njama ya kutoroka gerezani zaidi ya miaka minne iliyopita, wakati mtangulizi wake Hosni Mubarak alipopinduliwa.
Morsi tayari amehukumiwa kunyongwa
Mahakama inatarajiwa kutoa hukumu ya mwisho juu ya kesi hiyo baada ya mapumziko mafupi.
Mahakama imekuwa ikisubiri ushauri maalumu kutoka kwa kiongozi Mkuu wa Kidini nchini humo Mufti.
Kundi la Muslim Brotherhood lilitaja hukumu hiyo kama upuzi mtupu

Jumanne, 9 Juni 2015

KARDASHIAN FAMILY

Tazama hii picha ya baba na mama Kim Kardashian hajulikani mwanaume nani na mwanamke nani!!!halafu unasema Kim ni role model wako!

Jumatano, 3 Juni 2015

BOKO HARAMU WATOA ONYO JIPYA


Wanamgambo wa Boko haram wamekuwa tishio kaskazini mwa Nigeria
Wanamgambo wa kiislamu nchini Nigeria wametoa picha mpya za video lakini Kiongozi wa Boko Haram ambaye huwa anaonekana kwenye video zao, Abubakar Shekau hakuonekana kwenye picha hizo za video.
kutoonekana kwa Shekau kwenye Video hiyo kumeleta hali ya wasiwasi kuhusu kuwepo kwa hali ya mgawanyiko ndani ya kundi hilo.
Takriban watu 13 wameuawa siku ya jumanne katika shambulio la bomu katika Soko la Ng'ombe mjini Maiduguri, mji ambao uliwahi kuwa ngome ya Boko Haram, Kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Katika picha ya video ya dakika 10, msemaji huyo amekanusha taarifa zilizotolewa na Jeshi la Serikali kuwa linadhibiti miji yote kutoka mikononi mwa wanamgambo.
Ameonyesha vitambulisho vya wanajeshi akisema kuwa wameuawa, na kuonyesha mabaki ambayo amedai ya ndege ya kijeshi waliyoidungua.
Msemaji aliyekuwa amebeba bunduki na huku uso wake ukiwa umefunikwa, amesema video hiyo ilirekodiwa sambisa, msitu unaozunguka hifadhi.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari,amesema kuwa vikosi vya kijeshi viko kwenye doria mjini Maiduguri na kuhakikisha kuwaondoa wanamgambo hao katika eneo hilo.
Baadae wiki hii, Buhari atakutana na Viongozi wenzie wa nchi jirani kwa ajili ya kuzungumzia mikakati ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu.
Takriban watu milioni moja na nusu wamekimbia makazi yao, na mamia zaidi wametekwa tangu kuanza kwa harakati za kundi hilo mwaka 2009.
Zaidi ya Watu 15,500 wameuawa katika mapigano.
 
Shared directly from BBC SWAHILI.