Kurasa

Ijumaa, 24 Oktoba 2014

CHID BENZI AKAMATWA NA POLISI AKIWANA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anaefahamika kwa jina maarufu la CHID BENZ amekamatwa na polisi baada ya kukutwa na madawa ya kulevya katika mfuko wa shati lake alipokuwa anataka kupanda ndege kuelekea jijini mbeya kwaajiri ya Instagram party.

Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi Chid alikamatwa wakati anafanyiwa ukaguzi wa maungo yake kabla ya kusafiri katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Taarifa hizo zinadai kuwa Chid amekutwa na kete 14 za madawa ya kulevya ambayo bado yanafanyiwa uchunguzi kubaini ni aina gani ya madawa na misokoto miwili ya bange ambayo mwenyewe Chid amekiri kuwa ni yake na kusema kuwa ni kweli anatumia madawa hayo na anashangaa kwa nini aliyaweka katika mfuko wa shati.

Pamoja na madawa hayo Chid pia amekamatwa na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika uvutaji wa dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kigae na kijiko kilichokatwa.

Taarifa zinadokeza kuwa Chid anaendelea kufanyiwa uchunguzi na utakapokamilika basi atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabiri.

Katika safari hiyo Chid alikuwa na msanii mwenzake Shetta ambaye amefanikiwa kusafiri kuelekea katika tamasha hilo la istagram party wakate mwenzake Chid akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni