Kurasa

Jumanne, 2 Septemba 2014

SHUKRANI KWA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA TAASISI

Siku ya jumatano usiku ilikuwa ni siku ambayo niliuona kabisa mwisho wa mimi kuendelea kufurahia uumbaju wa Mungu katika dunia hii hasa pale nilipokuwa na saini kwaajili ya kufanyiwa upasuaji lakini kwa kwa nguvu zake ameniponya.NAMSHUKURU SANA MWENYEZI MUNGU KWA UPONYAJI WAKE HUU MKUU.

Katika mchakato huo Mwenyezi aliwatumia watu mbalimbali ambao sina budi kuwashukuru hapa kwasababu najua Mungu alikuwa na makusudio yake kuwatumia wao badala ya wengine:



Nimshukuru sana kaka yangu mpendwa,WILSON MUKEBEZI the pianist himself(waulize Makuburi),Mungu akubariki kazi za mikono yako mala nyingi zaidi ya sasa.HAKIKA I HAVE GOT BROTHER.

Nimshukuru kwa nguvu kubwa kabisa THE ONLY ONE IN MY LIFE JOYCE MATHEW.
Pole sana mama umekuwa na mimi katika kila hatua,umekuwa ukimlilia MUNGU aniponye,tumekesha pamoja nilipoumwa na tumbo usiku kucha na mengine mengi ambayo nikiandika hapa nitamaliza mwakani.ASANTE MUNGU KUNICHAGULIA WEWE.

Nimshukuru mama(mama credo).Nashukuru kwa nguvu nyingi ulizotumia siku ambayo jua lilikuwa linaonekana kuzama,ulipambana na hatimae limechomoza tena,Najua marehemu mama amefurahia sana kwa kuvaa viatu vyake.MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU.

Niwashukuru ndugu zangu waliopigana kwa namna moja au nyingine kuhakikisha kuwa narudi katika hali ya kawaida:
Dada Ester Mukebezi,Mama koku,Veronika Mukebezi,Maria Mukebezi,Baba na Bibi Mathew(wazazi wa mama Lai),prisca mdogo wake mama Lai,Baba Jose,Imma,Baba yangu mpendwa ambae amekuwa nae akifuatilia kwa ukaribu sana hali yangu mzee GORDIAN MUKEBEZI,mama angekuwepo mngefarijiana lakini maisha yana mengi

Familia ya Baba Meck,nawavulia kofia kwa upendo mlio nao,tunazunguukwa na majirani na marafiki wengi lakini kwangu you are the top.Ndugu jamaa na marafiki wote walionitembelea hospital,walionipigia simu,na walionitumia ujumbe Mungu awabariki sana.

Nitakuwa mchoyo wa fadhira nisipoishukuru HOSPITALI YA MASSANA hususani dactari wao PIUS pamoja na kitengo chote cha upasuaji kwa kazi yao nzuri kabisa,madaktari wengine ambao siwafahamu majina pamoja na wauguzi wote akiwepo Grol na Deo MUNGU aendelee kuwatia nguvu ya kuchapa kazi

Pia niishukuru hospitali ya wilaya Bagamoyo ambako nilianzia matibabu hususani manesi walioko wodi ya wanaume,nawashukuru kwa huruma mliyonionesha mpaka nilipoondoka ingawa mwishoni hali ya hewa ilionekana kuchafuka lakini mala nyingi ILI KIZURI KITOKEE LAZIMA KIBAYA KIWEPO NA UKIONA GIZA LIMEZIDI UJUE ASUBUHI IMEKARIBIA.

Bado naendelea kuuguza kidonda lakini kwa nguvu za Mungu mambo yanakwenda sawa na soon tutaungana katika michakato ya kimaisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni