Kurasa

Jumapili, 24 Agosti 2014

BWANA MAJENGO PENDA UNATAKA UKUU WA NCHI LAKINI???....

Du! Kweli hii balaaa,nimeona tena kwenye vyombo vya habari kuwa bwana MAJENGO PENDA kuwa na wewe umetangaza nia ya kutaka kuwa mkuu wa nchi hii!!.

Hahahaa hongera sana nafikiri inawezekana wewe kuwa mkuu wa nchi kwasababu una sifa ya kutokuwa na kashfa,huna makundi na una busara kiasi fulani ingawa umeshindwa kuukwepa mtego wa siasa za uchama.

Swali langu kwako mzee wangu ni kuwa je umejipanga kweli kupambana na kundi kubwa la watu zaidi ya kumi ambao nao wanawania nafasi hiyo akiwepo mheshimiwa mstaafu ambae sasa makanisa na misikiti vinafahamu pesa zake vya kutosha na anaonekana ameshaingia mpaka kwa wasanii kupata sapport??

Unaonekana kuwa na busara je utaweza siasa za kumwaga pesa kwa wananchi ili baadae ukipata uchukue chako mapema??

Waswahili wanasema ukiona panafuka ujue panaungua,na ukiona mtu anatangaza nia hadharani ujue tayari ameshajipanga kikamilifu,na ndio mana mimi nataka kugombea kama mgombea binafsi lakini sijatangaza nia bado kwasababu bado nakusanya signature! Lakini mzee wangu unahisi unaushawishi wa kutosha kweli kumzidi mheshimiwa ALIYELOWA SASA?.

Mhh mimi sijui bana labda ukiona au yoyote ayakaesoma hapa akikuambia kuhusu maswali yangu unaweza kuamua kunijibu kijana wako mana napata shida sana na huyo jamaa,hao wengine sina shida nao unaweza kuwapiga chini.

Hongera sana najua tutakutana kwenye kampeni mimi nikiwa mgombea binafsi na wewe ukigombea kwa tiketi ya CHUKUA CHAKO MAPEMA.SORRY.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni