Kurasa

Jumapili, 17 Agosti 2014

BWANA LESSO HILI LA URAIS UMECHEMSHA

Hahahaaa!Habariyako bwana Lesso.Niliona hivi karibuni umefunguka kwenye vyombo vingi vya habari kwamba chama chako cha Domo kikikuruhusu unataka kuwa kiongozi wetu wa nchi!!.
Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!usitake kunivunja mbavu!wewe ukakae Ikulu.Patakalika kweli??.
Najua katiba inasema kila mtanzania ana haki ya kuwa kiongozi,lakinipia usisahau kuwa kila mtanzania au binadamu ana kipaji chake na kwamba kuna eneo akikaa anafanya kwa ufanisi mkubwa.
Kwa maoni yangu wewe ufanisi wako uko mjengoni na huwa unachangamsha sana na kuleta changamoto uwapo pale mjengoni kwahiyo endelea kuwa pale kwasababu huku unakopataka hapakufai mjengo utapooza.
Hebu pata picha bila wewe nani atapiga kelele kule?au walinzi wa pale mjengoni watafanya kazi gani katika harakati za kutoa watu mjengoni.
Usifanye makosa aliyofanya mwenzako SULAA alipoamua kuacha mjengo na kutimkia urais wakati by then mjengo ullipamba moto.
Kumbuka mzee huyu alikuwa ukimuona na mkoba tu mjengoni ujue ana nyaraka anakuja kuripua jipu na mambo kweli yalikuwa yananyooka lakini mala baada ya kukosa u presidaaa mjengoni hayupo na wala hasikiki zaidi ya mitaani mpaka tunatamani arudi mjengoni.
Kwa hilli bwana Leso niseme kuwa umechemsha na upresidaa sio fani yako wewe endelea kufanya drama Bungeni na kuendelea kulichangamsha mambo yakae sawa.
Ni kwa nia ya kuwekana sawa kwahiyo usijenge chuki yoyote kwa kuwa mimi si mnazi wa chama chochote na haijulikani nani anafuata katika safu hii.tchao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni